ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 18, 2017

SNAPCHART YAFUNGA HUDUMA ZA AL JAZEERA NCHINI SAUDI ARABIA.

Mtandao wa kijamii wa Snapchat umefunga huduma za kituo cha Al Jazeera nchini Saudf Arabia.

Snapchat ilisema kuwa mamlaka nchini Saudi Arabia ziliiomba ifunge huduma za Al Jazeea kwa kuwa ilikiuka sheria za nchi hiyo.

Qatar inaendelea na mzozo yake na Saudi Arabia, Bahrain, Misri na UAE, Nchi hizo nne zilikata uhusiano na Qatar mapema mwaka huu na kuilaumu nchi hiyo kwa kuunga mkono Ugaidi.

Saudi Arabia ina moja ya sheria kali zaidi kwa vyombo vya habari, kwa mujibu wa makundi ya kutetea haki za binadamu.

Lakini kawaida Saudi Arabia haiipendi Al Jazera. Wakati mmoja waliitaka serikali ya Qatar ikifunge kituo hicho.



Saudi Arabia ni moja na masoko makubwa zaiidi ya mitandao ya kijamii eneo la mashariki ya kati itokanayo na matumizi makubwa ya simu za smart phone.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.