Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akipokea kombe la ushindi wa tatu
kutoka kwa Inspekta Hashim Abdallah wakati wa mapokezi ya wanamichezo wa Polisi
waliokuwa wakishiriki Michezo ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki
(EAPCCO Games) nchini Uganda .(Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimpongeza Mwanariadha wa Polisi PC
Basili John baada ya kushinda medali ya Dhahabu katika Michezo ya Majeshi ya
Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games) nchini Uganda hivi karibuni
ambapo Polisi Tanzania ilishika nafasi ya Tatu kati ya nchi saba zilizoshiriki
michezo hiyo.(Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimpongeza Mwanamichezo wa Polisi
Koplo Gaston Komba baada ya kushinda medali ya shaba kwa upande wa Taikondo
katika Michezo ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games)
nchini Uganda hivi karibuni ambapo Polisi Tanzania ilishika nafasi ya Tatu kati
ya nchi saba zilizoshiriki michezo hiyo.(Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro na Viongozi wengine wakiwa katika
picha ya pamoja na Wanamichezo wa Polisi walioshiriki katika michezo ya Majeshi
ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games) nchini Uganda hivi
karibuni ambapo Polisi Tanzania ilishika nafasi ya Tatu kati ya nchi saba
zilizoshiriki michezo hiyo.(Picha na Jeshi la Polisi)
POLISI WAREJEA NA MEDALI
MICHEZO YA MAJESHI.
Na. Jeshi la Polisi.
Wanamichezo
wa Polisi walioshiriki michezo ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za Afrika
Mashariki (EAPCCO Games) Kampala Uganda wamerejea nchini ambapo wamefanikiwa
kujinyakujilia jumla ya medali 6, 1 ya dhahabu, 2 za fedha na 3 za Shaba na
hivyo kuibuka mshindi wa tatu kwa ujumla katika michezo hiyo iliyoshirikisha
majeshi ya Polisi kutoka nchi saba.
Wanamichezo hao
wamepokelewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP
Simon Sirro ambapo alisema Jeshi hilo litaendelea kushiriki michezo mbalimbali
ili kujenga afya na ukakamavu kwa Askari pamoja na kuboresha mahusiano ya
utendaji kazi katika kubadilishana uzoefu na kuiletea sifa nchi.
IGP Sirro alisema
wanamichezo hao wamefanya kazi kubwa ambapo pamoja na uchache wao wameonyesha
kuwa wako vizuri katika michezo jambo ambalo ni hazina kubwa kwa Jeshi la
Polisi Tanzania.
Kwa upande wake
Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Ali Mussa alisema michezo hiyo imeliletea sifa
taifa la Tanzania na Jeshi la Polisi kwa ujumla hivyo kuna haja ya kuhakikisha
kuwa wanamichezo hao wanakaa kambini muda mrefu pindi itakapojitokeza michezo
mingine ili waweze kufanya vizuri zaidi.
Naye mshindi wa
medali ya Dhahabu katika riadha mita 800 PC Basil John amesema Michezo hiyo
ilikuwa na ushindani mkubwa lakini walijitahidi kupambana ili kuhakikisha
wanarejea na medali licha ya kuwa
wachache katika michezo hiyo ya majeshi ya Polisi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.