Kadhalika Spika wa Bunge Rebecca Kadaga ameagiza kutolewa kwa
nguvu nje ya majengo ya Bunge Waziri mmoja na Wabunge 25 wanaodaiwa
kuzusha vurumai juzi, aghalabu yao wakiwa wa upinzani.
Juzi wabunge wa chama tawala NRM na wale wa upinzani waliligeuza Bunge kuwa uwanja wa masumbwi na kutwangana makonde huku wengine wakirushiana viti.
Haya yanaarifiwa huku Kamisheni ya Mawasiliano ya nchi hiyo (UCC) ikisimamisha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

Godfrey Mutabazi, Mkurugenzi Mkuu wa UCC amesema idhaa au runginga
yoyote itayopeperusha matangazo ya Bunge mubashara itajiweka katika
hatari ya kupokonywa leseni, chini ya ibara ya 41 ya Sheria ya Kamisheni
hiyo ya mwaka 2013.
Museveni mwenye umri wa miaka 73, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi
ya miongo mitatu, kisheria hafai kuwania tena urais katika uchaguzi
mkuu wa 2021 kwa sababu katiba ya Uganda imeainisha miaka 75 kuwa kikomo
cha umri wa mtu anayetaka kugombea urais.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.