· Yasajili wateja wapya 132,826 kwa kipindi cha miezi mitatu
· Wateja wapya 1.038 milioni wa Airtel Money wasajiliwa
Airtel
Tanzania ndio kampuni ya simu za mkononi nchini Tanzania ambayo
imefanikiwa kuongeza wateja wengi kwenye robo ya pili ya mwaka huu huku
makampuni ya simu za
mkononi wakishindania kuongeza wateja wapya na watumiaji wa huduma za
kifedha kulingana na ripoti ya Tanzania Communications Regulatory
Authority (TCRA).
Kulingana
na ripoti ya robo ya pili ya 2017 (TRCA’s Quarterly Communication
Statistics Report), makampuni ya simu za mkononi Tanzania yaliongeza
watumiaji wapya wa
huduma za kifedha 1,059,163 milioni kwa kipindi cha April mpaka Juni.
Kutokana
na idadi hiyo, Airtel Tanzania ilisajili wateja wapya 1,038,193. Hii
inamaanisha ya kwamba kwa kipindi hicho asilimia 98 ya wateja wa huduma
za kifedha za
simu za mkononi wapya waliojiunga na Airtel Tanzania.
Akizungumza jijini Dar
es Salaam kuhusu mafanikio hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania
Beatrice Singano alisema ‘Hii ni ishara nzuri kuwa Airtel inatoa suluhisho
sahihi kwa huduma za kifedha kwa makampuni ya simu za mkononi hapa Tanzania.
Kwa mfano tuangalie huduma ya mikopo rahisi ya Timiza inayotolewa kupitia Airtel Money,
hatimaye imeanza kuzaa matunda’.
Huduma
ya mikopo ya Timiza inadhihirisha juhudi zetu za kutoa suluhisho
inapokuja suala ya huduma za kifedha kwa kutumia simu za mkononi. Pia
inaenda samba samba
na juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa wafanya biashara wadogowadogo
na wakati wanapata huduma ya mikopo yenye marshati nafuu, alisema
Singano.
Ikiwa
na ongezeko la 1.038 milioni, Airtel Tanzania kwa sasa ina jumla ya
wateja milioni 5.9 wa Airtel Money kwenye soko ambalo jumla ya makampuni
matano ya simu
za mkononi yanashindania wateja milioni 20. Airtel Tanzania pia
imefanikiwa kusajili laini mpya 132,826 kwenye robo ya pili ya mwaka na
hivyo kufikisha jumla ya watejakuwa milioni 10.3. Kwa ujumla, jumla ya
wateja wapya wa simu za mkononi waliongeza na kufikia
40.358 milioni mwishoni mwa mwezi Juni kutoka 39.856 mwishoni mwa Machi
mwaka huu.
Kwa kuendeleza uwekezaji zaidi nchini kwa mujibu wa Singano anathibitisha kuwa Airtel Tanzania inazidi kukua vizuri huku kampuni
hiyo ikiendelea kuwekeza zaidi kwenye miradi mbali mbali ili kufuta wateja
wengi wapya.
Moja ya mradi
mkubwa wa uwekezaji ni mradi wa U900.
Kulingana na Singano, Mradi wa U900 unatafuta kuboresha miundombinu ya
kiufundi kwa nia ya kuongeza kiasi cha data na kuboresha kasi ya data
"Hii
mikakati yetu ya kuimarisha maisha ya Tanzania kupitia huduma za
kidigitali. Katika jiji la Dar es Salaam zaidi ya maeneo 300 tayari
yamebadilishwa,
mpango wetu ni kueneza mradi wetu wa U900 kwa mikoa ya Mwanza,
Morogoro, Dodoma, Arusha na kisha katika masoko mengine yenye uwezo
mkubwa hapa nchini Tanzania, "aliongeza Singano.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.