Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mheshimiwa Mary Tesha akizugumza mara baada ya ufunguzi wa Tawi la UVCCM katika Stendi ya daladala Mwaloni maarufu kama Mererani, uzinduzi huo umefanywa na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Wakati wa Ziara ya kikazi Manispaa ya Nyamagana Mkoani Mwanza
Picha ya pamoja wadau wa tawi mara baada ya ufunguzi wa Tawi la UVCCM katika Stendi ya daladala Mwaloni maarufu kama Mererani, uzinduzi huo umefanywa na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Wakati wa Ziara ya kikazi Manispaa ya Nyamagana Mkoani Mwanza
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa Ofisi ya CCM Tawi la Bugarika Kaskazini
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na wanachama wa CCM maratu baada ya kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa Ofisi ya CCM Tawi la Bugarika Kaskazini
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) katika Picha ya pamoja na viongozi wengine wa Chama akiwemo Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula Mara baada ya kushirikiana ujenzi wa Ofisi ya CCM Tawi la Bugarika Kaskazini
Sasa ni mguu kwa mguu kushuhudia ujenzi wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha Mawe eneo la Bendera Mbili, Manispaa ya Nyamagana Mkoani Mwanza,
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana UVCCM
Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akishiriki ujenzi wa barabara
inayojengwa kwa kiwango cha Mawe Wakati wa Ziara ya kikazi Manispaa ya
Nyamagana Mkoani Mwanza, Kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Nyamagana
Mhe Stanislaus Mabula.
Ujenzi wa barabara
inayojengwa kwa kiwango cha Mawe unaendelea.Jumla ya vijana 500 wananufaika na ajira katika ujenzi wa barabara hii inayojengwa kwa kiwango cha Mawe Manispaa ya Nyamagana Mkoani Mwanza,
Ujenzi wa Barabara hii ya kiwango cha mawe unachukuwa urefu wa kilomita 2.5
Maelezo jinsi mawe yanavyopangwa.
Kabla ya hatua hizi za ujenzi wa barabara hii inayojengwa kwa kiwango cha mawe, wananchi wa vyombo vya usafiri walikuwa wakipita kwa kusua sua huku wakikutana na miamba iliyokuwa ikichelewesha huduma na maendeleo.
Eneo la kipande cha barabara ambacho kimekamilika hatua ya awali, hapa bado mawe tu.
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana CCM wilaya ya Nyamagana Hussein Kimu akitanabaisha miradi madhubuti waliyoibuni jimbo humo wakisaidiana na Mabula kwaajili ya kusaidia juhudi za kujikwamua na tatizo la ajira.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) hapa alikuwa akitia msisitizo. Pembeni yake ni Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula aliyeambatana naye kumwonyesha miradi mbalimbali ya maendeleo inayofanywa na vijana wa Jimbo lake.
Kaimu
Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akimsalimu mama Mlemavu
aliyekuwa akihitaji msaada katika eneo la Mtaa wa Pamba-Posta Wakati wa Ziara ya kikazi
Manispaa ya Nyamagana Mkoani Mwanza
Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa umesema kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM na Jumuiya zake zote hakiokoti wanachama barabani, uchochoroni, ama mtaani kama ilivyo katika vyama vingine ambavyo sio CCM.
Umoja huo umesema kuwa kuokota Viongozi barabarani ni kuzalilisha Chama na Jumuiya zake na kupoteza Misingi ya uwajibikaji na utendaji ya kupata viongozi walioandaliwa kuanzia ngazi ya Shina, Tawi, Mpaka Taifa.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Leo Julai 25, 2017 katika Ukumbi wa BELMOUNT FIRMOUNT HOTEL uliopo Manispaa ya Nyamagana Wakati wa ziara ya siku moja alipokuwa akizungumza na Vijana wa Jumuiya ya Chama hicho (UVCCM) pamoja na wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM).
Shaka alisema kuwa Chama cha Mapinduzi hufanya maandalizi ya uchaguzi Mkuu pindi tu unapomalizika uchaguzi kwa kuwapata Madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanza Kusimamia na kufatilia utekelezaji wa ilani ya ushindi ya CCM.
Alisema kuwa anavionea huruma vyama vya upinzani kwani havitaweza kuwa na mgombea Mwenye uwezo wa kushindana na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwani kazi kubwa anayoifanya nchini katika kipindi cha utendaji wake kinaungwa mkono na Wananchi wote wakiwemo wale wa Chama vya upinzani na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.
"Vijana wenzangu napenda mtambue kuwa siku zote Kizuri Chajiuza na kibaya chajitembeza, Hivyo Rais Magufuli ni KIZURI ambacho kinajiuza chenyewe bila hata kutembezwa na mtu yeyote" Alisema Shaka
Alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM kitaendelea kushinda kwa haki, Amani na Demokrasia pasina vurugu, Ghubu, na visilani kama inavyofanywa na vyama vingine visivyo CCM.
"Nataka niwakumbushe tu ndugu zangu wanachama wenzangu wa Chama Cha Mapinduzi CCM kuwa nchi yetu ya Tanzania haijawahi kuwa na vyama vya upinzani Bali imewahi kuwa na vyama vya vurugu na kejeli dhidi ya Serikali yao"
"Ninazo taarifa kuwa kuna Kata moja wamepitishwa wahenga kwenye uchaguzi wa Vijana sasa natoa maelekezo kwa Katibu wa UVCCM Wilaya ya Nyamagana na Mkoa wa Mwanza kusimamia na kuwatoa haraka kwani wakiwaacha mpaka wakaingia kwenye uchaguzi watakuwa wamekiuka taratibu na Kanuni za Uchaguzi" Alisisitiza Shaka
Katika Ziara hiyo Kaimu Katibu Mkuu huyo ameshiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Tawi la Bugarika Kaskazini na kuahidi kumalizia katika upauaji jambo ambalo limemfanya pia Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula kuchangia Bando tatu za bati ili kumuunga mkono Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka.
Aidha, Shaka ameshiriki ujenzi wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha Mawe yenye urefu wa Kilomita moja kwani itatoa urahisi wa Huduma za kijamii hususani kwa Wakati wa Kaya ya Mahina na Kata ya Pamba.
Shaka amesisitiza mipaka ya kazi na kuwepo heshima kwa kuchagua viongozi wenye sifa za kuchaguliwa huku akiwakumbusha Vijana Kujiunga katika vikundi Mbalimbali ambavyo watavisajili na hatimaye kuandika barua ya kuomba mikopo ambayo inatolewa na Serikali kwa riba nafuu ya shilingi 50,000 kwa kila wanapokopa Milioni Moja.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.