Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro na Meneja Mkuu wa kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Jianguo Liu wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari manne yaliyotolewa na kampuni hiyo ikiwa ni juhudi zake katika kulisaidia Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu nchini. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akisikiliza maelekezo ya jinsi inavyotumika moja ya magari manne waliyokabidhiwa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval. Anayemuelekeza ni Meneja wa Kampuni ya Kifaru, Mario Gaspari. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akikagua moja ya magari manne waliyokabidhiwa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval. Ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya kupambana na uhalifu. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akizungumza wakati wa Hafla ya makabidhiano magari manne yaliyotolewa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya kupambana na uhalifu. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay,jijini Dar es Salaam .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Meneja wa Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Jianguo Liu, akizungumza wakati wa Hafla ya makabidhiano magari manne yaliyotolewa na Kampuni hiyo ambapo aliahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya kupambana na uhalifu nchini.Kushoto aliyesimama ni mkalimani wa lugha ya kichina.Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini (IGP), Simon Sirro akipita mbele
ya magari manne yaliyotolewa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, ambapo
aliishukuru kampuni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya
kupambana na uhalifu.Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa
Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini (IGP), Simon Sirro (wanne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Meneja
wa Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Jianguo Liu(watatu kushoto), baada
ya makabidhiano ya magari manne kutoka kwa kampuni hiyo ikiwa ni mchango wao
katika kulisaidia Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu nchini.Wengine ni
viongozi wa juu wa jeshi na viongozi wa kampuni ya Haval.Hafla hiyo imefanyika
leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay,jijini Dar es Salaam
.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.