Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa, akifungua kikao hicho, pembeni kulia ni Mratibu wa LVEMP Bw. Omari Myanza.
Baadhi ya Viongozi wa dini kutoka mkoa wa kagera wakiwa katika Warsha hiyo.
Baba Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo katoliki Musoma Mkoani Mara
akiongea na Waandishi wa habari nje ya Mkutano huo kuelezea umuhimu wa
mazingira.
Sheik
Hassan Kabeke, akiafafnua jambo kwa waandishi wa habari nje ya Warsha
hiyo namna suala la mazingira linavyo tajwa katika Kuran tukufu.
Sheik
Hassan Kabeke, akiafafnua jambo kwa waandishi wa habari nje ya Warsha
hiyo namna suala la mazingira linavyo tajwa katika Kuran tukufu.
Mratibu wa LVEM Akitoa maelezo ya awali kabla yakuanza kwa Warsha hiyo
ilikutanisha Viongozi wa Serikali na Dini katika baadhi ya Mikoa ya
kanda ya ziwa (Picha zote na Ofisi ya mkuu wa Mkoa Mwanza).
Na
Atley Kuni- Mwanza.
Serikali
mkoani hapa, imewapa jukumu kubwa viongozi wa dini kutoka baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa kuhakikisha wanakuwa
bega kwa bega katika kulitunza ziwa Viktoria na Maliasili zake ili liweze kuwa
tegemeo kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Akifungua
Semina ya siku moja mkoani hapa Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, na risala
yake kusomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa, Mongella amesema,
viongozi wa dini wanalo jukumu kubwa kwani wao husimamia imani za watu. “Ninyi
Viongozi wa dini dhima mliyonayo ndani ya jamii ni kubwa sana na chochote
mtakacho waelekeza waumini wenu lazima waweze kukitekeleza, hivyo niwaombe sana
viongozi wangu tulilinde ziwa viktoria kwa jitihada zetu zote’’ alisema
Mongella.
Aidha
Mongella amesema kuwa, kuwepo kwa Ziwa Victoria ni fursa ya uendelezaji ya
kauli mbiu ya “Tanzania ya Viwanda”
ambayo Serikali ya awamu ya Tano inasisitiza,
“Ziwa hili linasaidia upatikanaji wa rasilimali zinazotumika kwa
matumizi ya nyumbani na viwandani, usafiri na usafirishaji na uzalishaji wa
nishati ya umeme Hivyo basi hatuna budi kuhifadhi mazingira ya Ziwa na Bonde
lake” amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.
Kwa
upande wao, viongozi wa dini wakiongea wamesema, wao wanatambua na hata vitabu
vya dini vinaelekeza juu ya mwanadamu anachopaswa kufanya katika kulinda
mazingira ikiwepo ziwa Viktoria.
Mwenyekiti
mwenza wa Kamati ya amani ya madhehebu ya dini katika Mkoa wa Mwanza, Sheik
Hassan Kabeke, amesema katika Uislam na
hususan ni katika mafundisho ya Mtume Muhama S.A.W, inafafanua juu ya mito miwili yaani mto Nile
na Furabu ambayo mtume aliipitia huku akisema kwamba, Mto Nile ambao
unafungamanishwa na Ziwa Viktoria Mtume amesisitiza kuyatunza mazingira,
“Katika kupanda miti kwenye uislamu mtu hupata thawabu, tunaimani kabisa kwamba
kila mmoja wetu akitunza mazingira ni sehemu ya Ibada, amesema Kabeke.
Naye
Baba Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo Katoliki la Musoma, kwa upande wake
amesema kwa habari ya mazingira, tunaona ni jukumu la jamii nzima bila kujali
itikadi zetu “ Kukutana kwetu hapa tunataka kuangalia nikwa namna gani
tutaziangazia sababu za kiuchumi na kijamii, alisema Msonganzila na kuongeza
kwamba kwa sasa wao katika Mkoa wa Mara wanayo kampeni kwenye eneo la Serengeti
ambayo wanaendelea kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa Utunzaji wa mazingira na
mabadiliko ya hali ya nchi.
Mradi
wa Hifadhi ya Mazingira wa Ziwa Victoria (LVEMP II) utakamilika mwezi Disemba,
2017, aidha warsha hiyo ni kati ya warsha nne zilizoandaliwa na Mradi kwa
madhumuni ya kukusanya maoni ya wadau ambayo yatawezesha kuandaa awamu ijayo ya
Mradi inayotarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2018.
Kikao
hicho kimewakutanisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa pamoja na
Viongozi wa dini kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Kagera, Simiyu na Mara.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.