Wito umetolewa kwa mawakili nchini kusimamia maadili
ya taaluma yao ili kutimiza majukumu yao kwa haki bila kujiingiza katika
migogoro na serikali.
Hayo yameelezwa na Rais wa Chama cha Wanasheria nchini
Tundu Lissu wakati wa ufunguzi wa mkutano
wao wenye lengo la kuwakumbusha mawakili wote nchini kusimamia maadili
ya taaluma yao pamoja na uhuru wa taaluma.
Lissu amesema kuwa endapo wakishindwa kuisimamia
taaluma hiyo na kuruhusu siasa ikaingia ndani yake basi haitokuwa na maana tena
kuwepo kwa chama hicho.
Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) kimeitisha mkutano wa dharura kujadili na kutoa msimamo wao juu ya mapendekezo ya Serikali kuanzisha Bodi ya Usajili wa Mawakili.
Akifungua mkutano huo leo (Ijumaa Juni 30) wenye lengo la kupata maoni ya wanachama, Rais wa TLS, Tundu Lissu amesema mapendekezo yaliyotolewa ni hatari kwa uhuru wa TLS na kada ya sheria kwa ujumla.
Amesema bodi hiyo ikianzishwa itakuwa chini ya waziri wa sheria na katiba na ndiyo itakuwa na nguvu ya kusajili au kuwafuta wanasheria kadri itakavyoona inafaa.
"Mabadiliko haya ni hatari sana kwa uhuru wa wanasheria nchini, tumekutana hapa kuelezana na kupokea maoni ya wanachama kisha tutaweka msimamo wetu baada ya baraza la TLS kukaa," amesema Lissu.
Lissu ambaye pia ni mbunge, amesema huo ni mkakati wa Serikali kuminya uhuru wa TLS ili kuwadhibiti wanasheria kuingia kwenye siasa, jambo ambalo anasema linatakiwa kupingwa na kila mtu kwa sababu matokeo yake ni mabaya.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.