Gazeti la serikali ya harare la The Herald limetangaza kuwa,
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa serikali ya Zimbabwe, Johannes Tomana
amefutwa kazi kutokana na mienendo isiyofaa na uzembe baada ya tume
iliyoteuliwa na Mugabe kutaka afukuzwe. Gazeti hilo limeongeza
kuwa, Johannes Tomana alikabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya ofisi na
madaraka yake.
Johannes Tomana alisimamishwa kazi kwa muda mwezi Februari 2016 baada kutupilia mbali mashtaka yaliyowasilishwa dhidi ya watu wawili waliotuhumiwa kupanga njama ya kulipua bomu kwenye kiwanda cha maziwa linachomilikiwa na mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe.
Rais Robert Mugabe na mkewe Grace Mugabe Duru za ndani ya Zimbabwe zinasema kuwa, sasa Johannes Tomana atakabiliwa na mashtaka ya kutumia vibaya madaraka yake.

Mivutano kati ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Zimbabwe na familia ya Rais wa nchi hiyo imekuwa ikiendelea kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja sasa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.