ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 29, 2017

MAKABURI MENGINE 10 YA ALAIKI YAGUNDULIWA MKOA WA KASAI KONGO DR, SERIKALI YANYOOSHEWA KIDOLE CHA LAWAMA.

Kamwina Nsapu, kiongozi wa waasi wa mkoa wa Kasai, Kongo DR.
Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Pier Numbi ametangaza habari ya kupatikana makaburi mengine 10 ya halaiki katika mkoa wa Kasai nchi humo.

Hii sio mara ya kwanza kwa mkoa huo kushuhudia makaburi ya namna hiyo tangu kulipoibuka mapigano makali baina ya askari wa serikali na wafuasi wa Kamwina Nsapu, kiongozi wa waasi wa mkoa huo aliyeuawa miezi michache iliyopita.
 
Mapigano hayo yalianza tangu mwezi Agosti mwaka jana wakati jeshi la nchi hiyo lilipovamia makazi ya kiongozi huyo wa waasi mjini hapo kabla ya kumuua.

WAKATI HUO HUO:-
 Mnamo tarehe 30 June 1960 koloni la Kongo ya kibelgiji wakati huo na sasa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilipata uhuru wake. Jembe fm kupitia mchakamchaka ya 93.7 kuanzia Leo tarehe 29 June 2017 imeliamsha kwa makala inayohusu uhuru wa nchi hiyo ya Afrika ya kati kesho mida ile ile saa 12:00 hadi 3:00 asubuhi ni muendelezo, kutana na wachapakazi @mackjumanne @jacquelineshuma @prince_nzwalla @stevedickenz & @deejaykflip @Jembefm Tupate popote ulimwenguni kupitia #tunein #googleplaystore search Jembe fm utupate LIVE™ 

CC:- @fallyipupa01 @koffiolomide_officiel @congotoglobal @zebingwa7777 @bellachristian1 @ferre_gola_officielle @awilolongomba @muanantsuka

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.