Timu ya soka ya taifa ya Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran imekuwa timu ya pili kujikatia tiketi ya michuano ya kombe la
dunia hapo mwakani huko nchini Russia baada ya kuigaragaza timu ya
Uzbekstan mbao 2 kwa nunge.
Ushindi wao uliwawezesha kufungua mwanya wa alama nane kati yao na wapinzani wao, ambao wamo nafasi ya tatu kwenye jedwali.
Wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya Iran wakishangilia baada ya mechi.
Mabingwa mara tano Brazil walikuwa taifa la kwanza kujiunga na
wenyeji Urusi katika kufuzu kwa michuano hiyo ya mwaka ujao nchini
Russia.
Timu mbili za kwanza katika kila kundi, kati ya makundi mawili ya kufuzu katika bara Asia zitafuzu, nazo timu zitakazomaliza nafasi ya tatu kila kundi zikutane katika mechi ya muondoano ya kufuzu.
Timu mbili za kwanza katika kila kundi, kati ya makundi mawili ya kufuzu katika bara Asia zitafuzu, nazo timu zitakazomaliza nafasi ya tatu kila kundi zikutane katika mechi ya muondoano ya kufuzu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.