Askari Polisi wawili wa
kikosi cha usalama wa barabarani wilayani Kibiti ambao majina yao bado
hayajatambulika wamepigwa risasi na watu wasiojulikana katika Kijiji cha
Msafiri,Kata ya Bungu wakiwa kazini.
Mbali na kupigwa risasi, pia watu hao wamechoma moto gari moja na pikipiki moja za askari hao kisha kutokomea kusikojulikana.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa tukio na kusema anafuatilia.
Tukio
hilo limetokea kilomita chache kutoka eneo ambalo waliuawa askari
polisi wanane kwa kupigwa risasi katika eneo la Mkengeni walipokuwa
wakitoka doria katika Kijiji cha Jaribu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.