FISTULA ni moja ya magonjwa yanayohatarisha afya ya mama mjamzito na mtoto kutokana na madhara yake endapo huduma ya haraka haitapatikana wakati wa kujifungua. United Nations Populations Fund UNFPA nchini Tanzania pamoja na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa pamoja vimeungana kuhakikisha ugonjwa huo unabaki historia nchini.
Kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya
kutokomeza Fistula ambayo huadhimishwa Mei 23 kila mwaka, Waziri wa Afya,
maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto, Ummy Ally Mwalimu ameitaka jamii
kuendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi za afya zinazotoa huduma ya matibabu ya
Fistula.
Waziri Ummy
ameihakikishia jamii kuwa serikali kupitia vizara yake imejipanga
kuboresha vituo vya afya 100 nchini ili viweze kutoa huduma ya upasuaji ya
dharura kwa wajawazito. Pia ameiasa jamii kuepuka vitendo vya ubaguzi kwa
wagonjwa wa Fistula.
UNFPA kupitia kwa mwakilishi wake nchini Hashina Begum, imesema
itaendelea kushirikiana na serikali pamoja na wadau wake kama Amref Health
Africa kuhakikisha huduma ya matibabu ya Fistula inawafikia wote wenye
matatizo. Hadi sasa UNFPA imefanikisha matibabu kwa jumla ya wanawake 85 elfu duniani kote.
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa CCBRT Erwin Talemans, amewataka
Watanzania kutoa ushirikiano kwa kuwafikisha wagonjwa katika vituo vinavyotoa
huduma ya tiba hiyo ikiwemo CCBRT Dar es Salaam na Bugando Mwanza pamoja na
Hospitali zingine nchini kama Mkinga iliyopo Tabora. Matbabu ya Fistula
yanatolewa bure pamoja na gharama zingine kama usafiri na Chakula.
FISTULA INATIBIKA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.