Abdul Hamis, aliyekutwa katika Kituo cha kupimia Mafuta cha Puma cha Jijini Mwanza, leo ikiwa ni siku ya Vipimo Dunian
Kinondoni, Maafisa wa Vipimo wa Kinondoni, wakiwa katika picha ya Mapoja leo ikiwa ni siku ya vipimo Duniani.
Gari la
Kubeba mafuta, likiwa linapita kwenye Mzani, leo ikiwa ni siku ya
Vipimo Duniani. (Picha zote kwa Hisani ya Wakala wa Vipimo nchini.)
Kamera ya Maafisa wa Vipimo, kama ilivyoshuhudia katika Eneo
la kukatia Tiketi za mabasi yaendayo mikoani Ubungo, kwenye eneo la
kupimia Vifurushi.
WAKALA WA VIPIMO (WMA)
SIKU YA VIPIMO DUNIANI
VIPIMO VINAVYOTUMIKA KATIKA
SEKTA YA USAFIRISHAJI
(MEASUREMENT FOR TRANSPORT)
Mei, 20 kila mwaka nchi nyingi duniani husherehekea siku
ya vipimo duniani. Mwaka huu kauli mbiu ( theme)
ya maadhimisho ni vipimo katika sekta ya usafirishaji (measurement for transport) .
Shirika la Vipimo Duniani (OIML) hutoa mapendekezo na miongozo ya kimataifa katika nchi
mbalimbali mojawapo ikiwa ni Tanzania kupitia Wakala wa Vipimo kuhusiana na
matumizi ya vipimo sahihi katika
biashara, na sasa tuko kwenye mpango wa kuingia katika sekta za afya, usalama na mazingira, nia na
lengo likiwa ni kuleta usahihi katika dhana nzima ya vipimo
kwa dunia nzima.
Hivyo, katika Sekta ya Usafirishaji kwa mfano ambayo ndio theme ya Siku ya Vipimo Duniani; Mizani
itumikayo barabarani, au kwenye viwanja
vya ndege au katika vituo vya mabasi ni
lazima ihakikiwe na kuthibitishwa na
Wakala wa Vipimo ili kupata usahihi wakati wa kupima uzito wa magari au
mizigo mbalimbali. Kama Mizani hiyo haitathibitiwa basi usalama wa wasafiri
pamoja na mizigo yao utakuwa mashakani. Vile vile, Vyombo vingi vya usafiri ili viweze kusafiri
kutoka sehemu moja kwenda nyingine huhitaji nguvu yaani mafuta au gesi. Mafuta
au gesi hutolewa kwa vipimo sahihi ili kuhakikisha chombo kinafika sehemu
sahihi kulingana na kiasi cha mafuta/gesi iliyochukuliwa kituoni. Vipimo
ambavyo vyombo vya usafiri (Ndege, Mabasi, Magari) huchukuwa mafuta/gesi ni
Vituo vya mafuta (Dispensing pumps) na Flow meters.
Kupitia Maadhimisho haya tutaeleza majukumu ya Wakala wa
Vipimo kwa ujumla na kubainisha umuhimu wa usahihi wa Vipimo nchini. Vile vile
tutajikita zaidi katika sekta ya usafirishaji ambayo ndio kauli mbiu ya
maadhimisho.
JUKUMU LA WAKALA WA VIPIMO TANZANIA
·
Wakala wa Vipimo
inalo jukumu la kumlinda mlaji na
umma kwa ujumla kupitia uhakiki na uthibiti wa vipimo vinavyotumika katika
biashara na huduma nyingine, kuhakikisha kuwa vipimo hivyo ni sahihi na
vinatumika kwa usahihi kulingana na Sheria ya Vipimo Sura 340 mapitio ya mwaka
2002 na maboresho yake ya mwaka 2016 pamoja na kanuni zake.
·
Hivyo,
Jukumu kuu la Wakala wa Vipimo ni kumlinda mlaji kupitia matumizi ya vipimo
sahihi.
KAZI ZA WAKALA
· Kuilinda jamii kutokana na madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya vipimo katika Sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira.
·
Kudhibiti
ufungashaji wa bidhaa (Net quantity &
lebelling)
·
Kuwa kiungo cha
Taifa letu na taasisi za Kikanda na Kimataifa katika masuala ya vipimo (legal Metrology)
·
Kutoa ushauri wa
kitaalamu kuhusu masuala ya vipimo kwa wadau
·
Kuhakikisha vifaa
vyote vitumikavyo nchini vinakuwa na ulinganisho sahihi na ule wa Kimataifa.
KAZI
ZA WAKALA WA VIPIMO KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI
Kuhakiki mizani mikubwa
inayotumika barabarani (Weighbridges/Axle
Weighers). Weighbridges ni mizani
zinazofungwa barabarani kwa ajili ya kupima uzito wa magari makubwa. Mizani
hizi hutumika kupimia magari ya kubebea mizigo/mabasi. Hufungwa barabarani kwa lengo la kupima uzito wa magari ili yasiharibu
miundombinu ya barabara yasisababishe ajali.
Kuhakiki mizani aina ya Platform, Counter Scales & Spring
Balances Mizani hii mara nyingi hutumika Airport, bandarini,
Posta na katika vituo vya mabasi kwa ajili
ya kupimia uzito wa mizigo inayosafirishwa katika sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
Vile vile Mizani hii hutumika Posta kwa ajili ya kupimia vifurushi mbalimbali
vinavyosafirishwa toka eneo moja kwenda eneo
jingine. Vifurushi hivyo hutozwa gharama za kusafirishia kulingana na
uzito wake. Mizani zote hizi yote upima uzito wa mizigo mbalimbali.
Kwa kutumia vipimo
hivi, wamiliki wa mizigo au wa vyombo vya usafiri hutozwa nauli za mizigo hiyo kulingana
na uzito wa mizigo husika. Pia, kutumia mizani katika vituo vya usafirishaji
hupunguza uwezekano wa kuzidisha uzito na kuepusha ajali za barabarani zinazotokana
na kuzidisha uzito.
Katika vituo vya
mafuta na bandarini kuna Dispensing pumps na Flow
meters, hivi ni Vipimo ambavyo vyombo vya usafiri kama Ndege, Mabasi,
Magari huchukuwa mafuta/gesi. Mafuta au gesi hutolewa kwa vipimo sahihi ili
kuhakikisha chombo kinafika sehemu sahihi kulingana na kiasi cha mafuta/gesi
iliyochukuliwa kituoni.
FAIDA ZA KUTUMIA VIPIMO KATIKA
SEKTA YA USAFIRISHAJI
A: Kuna faida mbalimbali zinazopatikana kwa kutumia
vipimo vya uzito katika sekta ya usafirishaji, baadhi ya faida hizo
ni pamoja na:-
i) Kulinda miundombinu ya barabara kupitia mizani
(Weighbridges) zinazofungwa barabarani.
ii) Husaidia kupunguza ajali barabarani kwa magari
yanayobeba mizigo.
iii) Husaidia wateja kutozwa ada ya mizigo/vifurushi
vinavyosafirishwa kulingana na uzito wa mzigo.
B: Vipimo vya kupimia
mafuta na gesi (Volume Measurements)
Vyombo
vingi vya usafiri ili viweze kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine
huhitaji nguvu yaani mafuta au gesi. Mafuta au gesi hutolewa kwa vipimo sahihi
ili kuhakikisha chombo kinafika sehemu sahihi kulingana na kiasi cha
mafuta/gesi iliyochukuliwa kituoni. Vipimo ambavyo vyombo vya usafiri (Ndege,
Mabasi, Magari) huchukuwa mafuta/gesi ni Vituo vya mafuta (Dispensing pumps) na
Flow meters.
Jaribu kufikiri kwa mfano ndege inaondoka ikiwa imepakia
abiria pamoja na mizigo na imejaza mafuta yakiwa pungufu yaani haijazingatia
matumizi sahihi ya vipimo ni dhahiri itakapokuwa angani itaishiwa mafuta, hivyo
usalama wake na wa abiria utakuwa mashakani. Hivyo, Vipimo vina umuhimu mkubwa
sana katika sekta ya usafiri.
C. Kipimo cha kupima mwendokasi (Speed Measuring Device)
Speed measuring device ni kifaa kinachotumika na Traffic kupima
speed (Mwendo kasi) wa magari yanayo tembea barabarani. Kifaa hicho hupima na kurekodi
mwendokasi wa gari linalokimbia barabarani. Faida ya kutumia vifaa hivi vya
kudhibiti mwendokasi ni dhahiri, mojawapo ikiwa ni kudhibiti ajali barabarani.
D. Vipimo vingine katika sekta ya usafiri
ambavyo Wakala wa Vipimo ipo kwenye mchakato wa kuvihakiki ni taximeter
pamoja na tyre pressure gauge.
CHANGAMOTO
i.
Upungufu wa
watumishi na vitendea kazi katika kufanya shughuli za vipimo.
ii.
Uelewa mdogo wa
sheria za vipimo kwa jamii ya wafanyabiashara na wananchi.
iii.
Kuwepo kwa mizani
mingi batili na isiyokuwa na ubora sahihi inayoingizwa nchini kinyemela na
baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu. Changamoto hii inasababishwa na
uhaba wa mizani nchini na hata ile michache inayopatikana/ kuagizwa toka nje ni
ghali kwa wananchi wa kawaida kumudu.
iv.
Uhaba wa Vipimo (hasa mizani) halali nchini.
Hivyo tukiwa tunaadhimisha Siku ya Vipimo Duniani ambayo
mwaka huu imejikita katika Sekta ya Usafirishaji, ni vyema tukatambua kuwa
umuhimu wa Vipimo sahihi uko katika kila
sekta ya maisha yetu hapa nchini. Baadhi ya sekta hizo ni kama Biashara, Afya,
Usalama, Mazingira na nyingine nyingi. Ni wajibu wetu pia kutambua kuwa Wakala
wa Vipimo ndio iliyopewa majukumu haya muhimu ya kumlinda mwananchi katika
harakati zake za kujenga uchumi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.