Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
ametengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi
Muhongo kuanzia leo tarehe 24 Mei, 2017.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza
kuwa nafasi ya Waziri wa Nishati na Madini itajazwa baadaye.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Wachezaji maarufu duniani waliokufa kwa ajali
-
Ulimwengu wa kandanda umekumbwa na ajali nyingi mbaya za magari kwa miaka
mingi, zikigharimu maisha ya vipaji vinavyoinuka na wataalamu waliobobea.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.