ZIMBWE JR, MSUVA KICHUYA NA MEXIME WANG’AA TUZO ZA
VPL 16/17.
Na Abog JEMBE FM.
Usiku wa kuamkia leo zimetolewa tuzo na zawadi kwa
washindi wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara VPL katika sherehe zilizofanyika
kwenye ukumbi wa Mlimani City.
Katika tuzo hizo, mlinzi wa kushoto wa Simba Mohamed
Hussein maarufu Zimbwe Jr ameibuka mchezaji bora wa ligi kuu msimu wa 2016/17.
Mabingwa wa ligi klabu ya Yanga wamekabidhiwa zawadi yao ambayo ni Tsh. Milioni
84, huku washindi wa pili,tatu na nne wakipewa zawadi zao ambao ni Simba, Azam
na Kagera Sugar.
Simon Msuva na Abdulrahman Mussa pia wamekabidhiwa
zawadi yao ya ufungaji bora. Tuzo ya kocha bora imechukuliwa na kocha wa Kagera
Sugar Meck Mexime huku mshambuliaji wa klabu hiyo Mbaraka Yusuph akiibuka
mchezaji bora chipukizi.
Golikipa bora ni Aishi Manula wa Azam huku Shiza
Kichuya akitwaa tuzo ya goli bora alilofunga dhidi ya Yanga kwenye mechi ya mzunguko
wa kwanza. Tuzo nyingine ni ile ya mchezaji bora wa kigeni ambayo imetua kwa
kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima, huku tuzo ya heshima ikitua kwa Kitwana
Manara.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.