Tayari Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na hii hapa taarifa kamili. BOFYA VIDEO KUIPATA TAARIFA KAMILI.
Mwanza. Mkazi wa Mahina, jijini Mwanza, aliyefahamika kwa jina moja la Max, anadaiwa kumuua mke wake, Teddy Malulu kwa kumpiga risasi usiku wa kuamkia leo.
Baada ya kufanya mauaji hayo, Max naye anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi. Mpaka sasa chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa mwanamke anayedaiwa kuuawa na mume wake ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi Tanzania (Tafu) .
Kamanda Msangi amesema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea. Taarifa kamili na #video nimeiweka
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.