Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja
Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu (aliyevaa Kaunda suti) akiwasili
katika Viwanja vya Kyaikarabwa kutembelea na kukagua shughuli
zinazoendelea wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa inayofanyika
kitaifa mkoani Kagera.
Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu akikaribishwa katika Banda la
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TABD, Bw. Saidi Mkabakuli.
Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja
Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu (aliyeshika kipaza sauti kulia)
akizungumza wakati alipotembelea Banda la TADB. Anayemsikiliza kushoto
ni Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TABD, Bw. Saidi Mkabakuli.
Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja
Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu akimsikiliza Afisa Mahusiano na
Masoko Mkuu wa TABD, Bw. Saidi Mkabakuli wakati alipotembelea Banda la
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwenye Viwanja vya
Kyaikarabwa yanapofanyika Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa mkoani Kagera.
Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TABD, Bw. Saidi Mkabakuli akisisitiza jambo wakati Mkuu
wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu (hayupo pichani) alipotembelea Banda la TADB.
Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu amewaasa
wakulima na wafugaji
wa mkoa wa Kagera kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kujikwamua katika shughuli zao
za kilimo mkoani humo.
Meja Jenerali (Mstaafu) Kijuu alitoa wito huo alipotembelea Banda la TADB wakati wa Maadhimisho
ya Wiki ya Maziwa inayofanyika kitaifa mkoani Kagera.
Mkuu wa mkoa huyo alisema
kwa kuzingatia malengo ya uanzishwaji wa Benki ya Kilimo unalenga
kutimiza dhamira ya Serikali ya kuwasaidia wakulima nchini kote
kukabiliana na mapungufu kwenye kuongeza tija katika shughuli zao za
kilimo.
“Nawaomba wakulima na
wafugaji wa Kagera kuchangamkia mikopo nafuu ya Benki yetu ya Kilimo
ili muongeze tija katika kilimo chenu maana Benki ipo kwa ajili ya
kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza
mapinduzi katika
kilimo nchini,” Meja Jenerali (Mstaafu) Kijuu alisihi.
Kwa mujibu wa TADB, sekta za kilimo na mifugo ni sekta za kipaumbele ambazo zinazopatiwa mikopo
kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo hasa katika uongezaji wa thamani wa sekta hizo nchini.
Benki hiyo inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya Muda Mfupi
(Hadi Miaka Miwili (2)),
Mikopo ya Muda wa Kati (Zaidi ya Miaka 2 hadi Miaka Mitano (5)) na
Mikopo ya Muda Mrefu (Zaidi ya Miaka 5 hadi Miaka Kumi na Mitano (15)).
TADB ni taasisi ya serikali
ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa upatikanaji
wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao ulikuwa
unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha
kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye
mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti
magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo
na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.