Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga akizungumza juu ya umuhimu wa wadau katika kuchagiza uwekezaji katika sekta ya kilimo nchini.
Mkuu wa Kilimo na Fedha Vijijini wa FSDT, Bw. Mwombeki Baregu (Kulia) akizungumza wakati wa mkutano huo. Pichani ni Mwenyekiti wa Kikundi Kazi, Bw. Peniel Lyimo (Katikati) na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.
Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB, Bw. Albert Ngusaru akiwasilisha malengo ya mkutano huo.
Waumbe wa Kikundi Kazi cha Kuchagiza Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo nchini wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa.
Waumbe wa Kikundi Kazi cha Kuchagiza Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo nchini wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya FSDT, Balozi Mwanaidi Maajar (Kulia) akitoa mchango wakati wa
Kikao Kazi cha Kuchagiza Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo nchini. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji
Fedha wa TADB, Bw. Albert Ngusaru.
Mjumbe
wa Bodi ya Wadhamini ya FSDT, Balozi Mwanaidi Maajar (Kushoto)
akifurahia jambo na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (Kulia) wakati wa
Kikao Kazi cha Kuchagiza Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo nchini.
WADAU WAKUTANA KUCHAGIZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA KILIMO
Na Mwandishi wetu
Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kushirikiana na Mfuko wa
Kukuza Sekta ya Fedha (FSDT) imewakutanisha pamoja wadau
kutoka sekta mbalimbali za maendeleo nchini kujadili masuala mbalimbali
yatakayosaidia uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo Tanzania.
Akizungumza katika kikao kazi hicho mwenyekiti wa Kikundi Kazi, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Peniel Lyimo
alisema kuna haja ya dhamira ya dhati na
uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo nchini ili kusaidia juhudi za
Serikali za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini.
Bw.
Lyimo alisema kuwa ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa
ajili ya maendeleo ya kilimo nchini unachangiwa kwa kiasi
kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye
upande wa biashara za bidhaa hali inayorudisha nyuma mapinduzi katika
sekta ya kilimo nchini.
“Kuna
haja ya kutafuta suluhisho la changamoto za upatikanaji wa fedha mikopo
kwa ajili ya Kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo
kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye
ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.
Akizungumzia
umuhimu wa kikao kazi hicho, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw.
Francis Assenga alisema kikao hicho kinalenga kuwaleta
wadau kutoka sekta mbalimbali ili kujadili kwa kina njia sahihi za
kuchagiza uwekezaji wenye tija katika kilimo nchini.
Bw. Assenga alisema kuwa kwa kushirikiana
na wadau mbali mbali wa maendeleo kutachagiza kusaidia uwekezaji mkubwa
kwenye Sekta ya Kilimo, na kuleta mapinduzi ya kilimo nchini.
“Kimsingi Kikao hiki kinalenga kuanzisha
mtandao mpana wa majadiliano na
wadau mbalimbali, zikiwemo Wizara zinazohusika na Kilimo na Taasisi
mbali mbali za Serikali na Binafsi, ili kukubaliana vipaumbele na namna
ya kushirikiana katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya TADB
katika kuleta mapinduzi ya kilimo nchini,” alisema
Kwa
upande wake, Mkuu wa Kilimo na Fedha Vijijini wa FSDT, Bw. Mwombeki
Baregu alisema kuwa
FSDT inalenga kushirikiana na wadau ili kuchagiza ushirikishaji mpana
wa washirika mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ili kuongeza
uwekezaji katika sekta ya kilimo nchini.
“Miongoni
mwa vikwazo katika kufikia ushirikishwaji wa fedha nchini Tanzania hasa
katika uwekezaji
katika kilimo ni pamoja na ukosefu wa miundombinu sahihi ya soko na
upatikanaji wa fedha na huduma na bidhaa zake maalum katika kilimo,
hivyo tunaamini kwa kushirikiana na wadau tunaweza kutatua changamoto
hizi,” alisema Bw. Baregu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.