Operesheni maalum ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali inaendelea kutekelezwa nchini kote kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya pamoja na Kamati za Mazingira za Mikoa na Wilaya. Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa zinawajibika kuwasilisha taarifa za operesheni wakati na baada ya operesheni hiyo Ofisi ya Makamu wa Rais. Majumuisho ya taarifa ya nchi nzima yatafanywa baada ya Kikosi Kazi kuendesha Operesheni maalum katika Jiji la Dar es Salaam kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 01 hadi 03 Machi 2017. Operesheni hii inatokana na kuwepo kwa Viwanda vingi na wasambazaji wengi wa Pombe kali aina mbalimbali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (sachets).
Ofisi ya Makamu wa Rais iliratibu
operesheni maalum katika Jiji la Dar es
Salaam kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 01 hadi 03 Machi 2017. Operesheni
hii ilitokana na kuwepo kwa viwanda
vingi vinavyozalisha pombe kali za aina mbalimbali zilizofungashwa katika
vifungashio vya plastiki (sachets)
ambazo hazikidhi vigezo mbalimbali vya Sheria.
Kikosi Kazi maalum katika Operesheni
hii tulikielekeza kufanya yafuatayo:-
i)
Kukagua na kuzuia (seize) pombe kali
zilizofungashwa katika viroba (sachets) kwenye viwanda na kuorodhesha idadi ya
pombe za viroba zilizopo, vifungashio (packaging materials), mitambo mahususi
kwa ajili ya kufungashia pombe za viroba na mitambo ya kutengeneza vifungashio;
ii)
Kukagua na kuzuia pombe kali
zilizofungashwa katika viroba (sachets) kwenye maghala (warehouse /store), na
maduka ya jumla (whole sale) na kuorodhesha idadi ya pombe kali zilizofungashwa
katika viroba na vifungashio (packaging materials) tupu vilivyopo;
iii)
Kubaini iwapo kuna mapungufu yoyote
kwenye ufungashaji pombe kali;
iv)
Kukagua viwanda vya kutengeneza
vifungashio vya sachets kubaini kama kuna ukiukwaji wa Sheria;
v)
Kukagua uhalali wa vibali na nyaraka za
uzalishaji / uendeshaji wa kiwanda / msambazaji husika (mfano vibali na vyeti
vya TFDA na TBS, EIA, stempu za kodi za TRA, leseni za biashara, leseni za
vileo);
vi)
Kukagua nyaraka zinazoonesha kumbukumbu
za uzalishaji na nyaraka za usambazaji (sehemu bidhaa zilipouzwa kwa jumla) ili
kujua kama uzalishaji na usambazaji unafanyika;
vii)
Kufanya tathmini ya Operesheni, kuboresha
mapungufu na kuandaa ripoti ya Operesheni; na
2. UKAGUZI ULIVYOFANYIKA
Jumla ya wakaguzi 58 walishiriki katika zoezi hili na
kugawanywa katika timu tatu (3) kulingana
na mikoa ya kikodi ya TRA Dar es Salaam, ambayo ni Temeke, Kinondoni na Ilala.
Aidha, timu hizo pia zilijumuisha askari polisi na wanahabari.Katika operesheni
hii, TFDA na TBS waliainisha viwanda vinavyozalisha pombe kali, na Manispaa
ziliainisha maduka, maghala na baa zinazofanya biashara ya pombe kali
kinyume na sheria.
Sheria
mbalimbali za udhibiti ikiwa ni pamoja na Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi
Sura, 219; Sheria ya Viwango Namba 2 ya mwaka 2009, Sheria ya Vileo ya mwaka
1968 (ilirejewa mwaka 2012), Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura, 191 na
Kanuni ya Kukataza Uzalishaji, Uingizaji na Matumizi ya Vifungashio vya
Plastiki kufungia Pombe Kali, iliyochapishwa katika Gazette Serikali Namba 76
ya mwaka 2017 zilitumiwa katika kutekeleza Operesheni hii.
3. MATOKEO YA UKAGUZI
Jumla ya
viwanda 16 vya kuzalisha pombe kali,
maduka ya jumla 18, maghala manne,
baa tatu na kiwanda kimoja cha kuzalisha bidhaa za plastiki
ikiwemo vifungashio vya plastiki vya kufungashia pombe kali (viroba)
vilikaguliwa ambapo matokeo ya ukaguzi ni kama ifuatavyo:-
(i)
Jumla ya carton 99,171 za pombe kali zilizofungashwa kwenye
vifungashio vya plastiki (viroba) zimekamatwa
Kati yake vyenye ujazo wa mililita 50 ni carton 69,045 na milita 100 ni
carton 29,344 za milliita 90 ni 782
Aidha, chupa zenye ujazo wa mililita
100 ni 10,625. Thamani yake ni Tshs bilioni 10.83
(ii)
Chapa mbalimbali za pombe kali za virobakama vile
Red Wine, Banjuka, Officer’s Cane Spirit, Flash Ginna Dragon zilikuwa hazikidhi viwango na zilikuwa
hazijasajiliwa na TFDA hapa nchini
(iii)
Makampuni yote yaliyokamatwa hayana Vyeti vya
Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA). Makampuni mengine yalikuwa hayajalipa
kodi TRA na hayakuwa na cheti cha TFDA
na wala cheti cha TBS.
(iv)
Makampuni mawili yalikutwa yanazalisha na kusafirisha mizigo
usiku
(v)
Viroba vyenye thamani ya jumla ya Tshs 235
millioni vimekutwa vimefichwa kwenye
maghala ya duka la jumla chini ya jengo la ghorofa (handaki) Kariakoo.
(vi)
Baadhi yapombe kali aina mbalimbali
zilizofungashwa katika viroba na chupahazikuwa na namba ya matoleo (batch
numbers) na tarehe za uzalishaji kwenye lebo (label);
(vii)
Baadhi ya pombe kali zilizoonekana wakati wa
ukaguzi wa viwanda, maghala, baa na maduka ya pombe kali hazikuwa na stickers sahihi
za TRA na nyingine zilikuwa na stickers ambazo zilihisiwa na TRA kuwa bandia, na hivyo kuhitaji uhakiki zaidi;
(viii)
Viwanda saba (7) vilikutwa vinafanya marekebisho kutokana na kusimamishwa
awali na TFDA kwa kosa la kutoweka
kabisa namba za matoleo na tarehe ya kuzalishwa kwa bidhaa au kuweka taarifa
husika katika bidhaa chache walizozalisha hadi hapo watakapokidhi masharti ya
TFDA;
(ix)
Baadhi ya pombe kali kwenye baadhi ya viwanda, maghala,
maduka na baa zilikuwa zimefungashwa kwenye chupa zenye ujazo wa chini ya
mililita 200 ambavyo ni rahisi kubebeka kama viroba.
4. HATUA ZILIZOCHUKULIWA
Hatua
mbalimbali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na:-
(i)
Bidhaa za pombe kali zilizofungashwa
katika vifungashio vya plastiki zenye ujazo mdogo zenye thamani ya takriban Tshs 10.8 billionizimekamatwa na kuzuiliwa
(seized) katika store za viwanda, maduka ya jumla, baa na maghala ya
wasambazaji;
(ii) Idara
ya Uhamiaji imeagizwa kushughulikia raia wa kigeni wasio na vibali vya kuishi
nchini ambao walikutwa kwenye baadhi ya viwanda wakati wa ukaguzi;
(iii) Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeelekezwa kuvifuatilia
na kuvichukulia hatua viwanda vyote vilivyokaguliwa na kugundulika kufanya kazi
bila kuwa na cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Environmental Impact
Assessment) au Cheti cha Ukaguzi wa Mazingira (Environmental Auditing);
(iv) Mamlaka
ya Mapato Tanzania imelekezwa kufuatilia na kuchukua hatua stahiki kwa viwanda
na maghala yote yaliyoonekana kuwa na bidhaa zenye stickers za TRA
zinazosadikika kuwa bandia.
(v) TFDA
na TBS wameelekezwa kufuatilia kwa karibu usitishaji wa ufungashaji wa pombe
kali katika mifuko ya plastiki (viroba) na
na chupa za ujazo mdogo chini ya 200mls; na
(vi) Bidhaa
zote zilizokamatwa zitabaki hivyo hadi Serikali itakapoelekeza hatua ya baadae.
5.
HATUA ZINAZOFUATA
(i)
Kuendelea na na Operesheni hii nchi
nzima kwa kasi zaidi. Aidha, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mkoa,
Wilaya hadi ngazi ya Vijiji zihakikishe
agizo hili linatekelezwa nchini kote. Wenye viti wa Mitaa na vijiji
wahusike pia kwa kushirikiana na kamati hizi. Aidha, Kamati za Ulinzi na
Usalama za Mikoa zinawajibika kuwasilisha taarifa za operesheni wakati na baada
ya operesheni Ofisi ya Makamu wa Rais kila mara kwa kufuata maelekezo
yatakayotolewa.
(ii)
Kufungua kesi mahakamani dhidi ya
wafanyabiashara waliokiuka katazo hili ili adhabu kali kutolewa
(iii)
Viroba vyote vilivyokamatwa pamoja na mizigo mingine itabaki chini ya
ulinzi kwa sheria zilizotumika na mtu yeyote haruhusiwi kufanya chochote hadi
maelekezo zaidi yatakapotolewa na serikali.
(iv)
Kwa walioomba muda wa nyongeza kuhamia kwenye
teknolojia ya chupa, maombi hayo yatashughulikiwa baada ya Operesheni ya
kuondoa pombe kali ambazo zimezalishwa na zinauzwa kinyume cha Sheria.
6. WITO
Operesheni ya
utekelezaji wa kuzuia uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio
vya plastiki nchini ni endelevu na ina lengo la kuimarisha afya ya jamii,
kudhibiti ukusanyaji wa mapato na hifadhi ya mazingira kwa vizazi vya sasa
na vijavyo. Katika kutimiza azma ya operesheni natoa wito ufuatao: -
(i)
Kila mwananchi ashiriki katika
utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kwa
kutoa taarifa zitakazowezesha kubaini wanaokaidi agizo la Serikali la kuzuia
uzalishaji, usambazaji na matumizi ya pombe kali zinazofungashwa katika
vifungashio vya plastiki na katika ujazo mdogo. Zawadi itatolewa kwa watakaotoa
taarifa ya wanaohusika na tutahakikisha usiri wa hali ya juu;
a. Kwa
atakayetoa taarifa itakayowezesha kukamatwa na kushtakiwa mtu anayezalisha,
anayeuza au kutumia stempu feki za TRA, atapata zawadi ya shilingi milioni
moja;
b. Mtu
atakayetoa taarifa itakayowezesha kukamatwa na kushtakiwa mtu yoyote mwenye
kiwanda/mtambo wa kuzalisha pombe za viroba ambao hautambuliki na Serikali au
mwenye mtambo wa kutengeneza viroba au kuchapisha chapa za viroba kinyume na
sheria, atapata zawadi ya shilingi milioni moja.
c. Mtu
yoyote atakayetoa taarifa itakayowezesha kukamatwa na kushtakiwa mtu yoyote
mwenye ghala au aliyehifadhi shehena ya pombe za viroba kinyume cha Sheria
atapata zawadi ya shilingi laki 5.
d. Mtu
yoyote atakayetoa taarifa ya kuwezesha kukamatwa kwa mtu au watu wanaoingiza
nchini pombe za viroba kutoka nje ya Tanzania kinyume na Sheria na utaratibu
atapata zawadi ya shilingi laki 5.
e. Mtu
yoyote atakayetoa taarifa ya kuwezesha kukamatwa na kushtakiwa mtu yoyote
anayehamisha au kusafirisha pombe za viroba kinyume na Sheria na maelekezo ya
Serikali atapata zawadi ya shilingi laki 5.
Taarifa hizi zitolewe
kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) au Whatsapp au kwa kupiga simu kwenye simu
nambari 0685 333 444 au kwa Afisa
yoyote kwenye Operesheni hii.
(ii)
Wafanyabiasharana wananchi waliokuwa
wanajihusisha na uzalishaji, usambazaji, uuzaji na uingizaji wa pombe kali
zinazofungashwa katika viroba wanatakiwa kutii
maelekezo haya ya Serikali mara moja;
(iii)
Taasisi za TFDA, NEMC na TBS zinaelekezwa
kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ili kufikia
malengo yanayotarajiwa; na
(iv)
Serikali za Mitaa kupitia Wenyeviti na
Watendaji wa Vijiji / Mtaa na Kata washiriki katika kuwatambua na kutoa taarifa
ya watu au kikundi cha watu wanaojihusisha na uzalishaji, usambazaji, uuzaji na
matumizi ya pombe kali zilizifungashwa katika viroba; na
(v)
Kuhakikisha wafanyabiashara wote
waliokamatwa na watakaokutwa wameshindwa kulipa kodi wanalipa kodi stahiki mara
moja.
January
Makamba (Mb)
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
5
Machi 2017
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.