Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali
katika Ibada ya Jumatano ya Majivu pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya
tatu Benjamini Wiliam Mkapa, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na
Mke wake Mama Janeth Magufuli katika Kanisa Katoliki Parokia ya
Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akijiandaa
Kumpaka majivu kichwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli katika Ibada ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika
katika Kanisa Katoliki Parokiya ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay
jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam
Mkapa mara baada ya Ibada hiyo ya jumatano ya Majivu iliyofanyika katika
Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam. PICHA NA
IKULU
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.