ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 21, 2017

LISSU: NI WAKATI WANGU KUWA RAIS

NA ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza

MGOMBEA urais chama cha wanasheria nchini (TLS) na Wakili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Tundu Lissu amesema haki za kisheria inamruhusu kugombea wafidha huo.

Akizungumza jana na waandishi wa habari nje ya Mahakama Lissu ameeleza kuwa uanachama wake wa chama cha wanasheria kutokana na ada alizolipa unamruhusu kugombea na kwamba Sheria haijakataza kuwa mwanasiasa haruhusiwi kugombea.

“Watu wanaoleta hoja za mimi kutogombea kama ni wanasheria basi hawajui kutumia uwana sheria wao vizuri, kwanza hiki ni chama cha wanasheria  Tanganyika (KLS) na sio Tanzania  Low Society, ukiwa mwanachama wa cha wanasheria unatakiwa kulipa kodi,na ada na sheria hii haijakataza mimi kugombea eti kwa sababu ni mwanasiasa” amesema Lissu.

Aidha ameeleza kuwa chama cha wanasheria (TLS) kimepotea kwani wao ndio wanatakiwa kusimamia na kushughulikia  haki na kwamba huenda anaogopwa kutokana na misimamo yake ya kikatiba.

“Ni wakati wa kuwa Rais wa TLS ili kukisimamia chama hiki kwa kufuata haki kwa mujibu wa sheria na kusimamia sheria mbovu zinazotungwa, mtu anaetakiwa kujua sheria kuliko mtu yeyote yule ni mwana sheria wao ndio wanatakiwa kujua sheria zinasemaje.”

Hata hivyo amesema kuwa endapo chama hicho kitafutwa  inamaana hakutakuwa na wakili, na mambo yote yanahitaji watu kama hao hayataweza kufanyika kutokana na kwamba ili kuwa mwanasheria katika nchi hii ni lazima uwe mwanachama wa TLS. GSENGO BLOG

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.