ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 23, 2017

GEITA:NHIF YAKUTANA NA WADAHU NA KUHAIDI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA.

Mwenyekiti wa Bodi NHIF  na Spika mstaafu wa Bunge mama Anna Makinda akisisitiza juu ya huduma kuboreshwa katika mfuko wa Bima ya afya wa Taifa. 

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwa na mwenyekiti wa Bodi ya NIHF wakisikiliza kwa makini taarifa ya Mkoa wa Geita juu ya mfuko wa bima ya afya .

Mbunge wa Geita Mjini Constatine Kanyasu na Mbunge wa Jimbo la Busanda  Lorencia Bukwimba wakifatilia mkutano .

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu  Ezekiel Kyunga akifungua mkutano wa wadau wa Mfuko wa Bima wa Taifa Mkoani Humo.

Mbunge wa Geita Mjini Constatine Kanyasu,akielezea namna ambavyo kumekuwepo na changamoto za huduma ya afya katika jimbo ambalo analiongoza.

Mbunge wa Bukombe  Dotto Biteko akichangia swala la huduma ambazo zinatolewa na mfuko wa Bima ya afya wa NHIF.

Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye kikao wakisikiliza taarifa ya utekelezaji wa shughuli za NHIF.

Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Angela Mziray akifafanua namna ambavyo NHIF imekuwa ikisaidia wa gonjwa wenye magonjwa yasiyoambukiza.
Na Joel Maduka  
KUTOKANA na kuwepo kwa baadhi ya vituo vya afya kuwa na mazingira yasiyo mazuri ya kimiundombinu  na  lugha chafu kwa baadhi ya hudumu wa afya,ukosefu wa dawa na upungufu wa wataalam imeelezwa kuwa chanzo ambacho kimekuwa kikisababisha juhudi za wananchi kutokujiunga  na mfuko wa Bima ya afya .


Akizungumza  katika mkutano wa wadau wa afya Mkoani Geita mwenyekiti wa Bodi NHIF  na spika mstaafu wa Bunge Anna Makinda amesema wanafanya maboresho ya kuhakikisha kila atakayejiunga  awe na uwezo wa kupata huduma kuanzia ngazi ya kijiji hadi Mkoani hivyo watumishi wachache wasiharibu fursa ya wananchi kupata huduma nzuri.

“Inatakiwa mtu ambaye anakata NHIF aende akatibiwe kwenye ngazi ya zote ndani ya Mkoa sio haishie kwenye zahanati ,zahanati zingine zimekuwa zikikatisha tama unakuta mganga hayupo hata dawa hazipo jambo ambalo limekuwa likiwakatisha tamaa wananchi ninachokisema wakurugenzi zungumzeni na wananchi harafu tushirikiane katika mambo yafatayo lazima dawa ziwepo kituo cha afya kiwe kituo cha afya kweli Mganga mkuu nadhani yupo hakikisha unafatilia haya mambo kwa umakini zaidi”Alisema Mama Makinda

Hata hivyo kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa NHIF Angela Mziray ameongezea kuwa Bado wananchi wanakabiliwa na magonjwa ambayo elimu hawana na ukiangalia mfuko unaingia gharama ya asilimia 19 kutibu magonjwa yasiyoambukiza.

“Kutokana na mtinda wa maisha ambayo tumekuwa tukiishi kila siku unajikuta magonjwa ya siyoambukizwa yamekuwa yanaongezeka kwa kiasi kikubwa sana sasa kutokana na hili mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya iliona ni vyema ukaboresha kwa kughalamia  asilimia 19 za matibabu kwa mgonjwa” Alifafanua Mziray.

Mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali  Mstaafu Ezekiel Kyunga  amewasisitiza watumishi wa sekta ya afya kuakikisha wanakuwa na maadili ya kazi zao na kuachana na tabia ya ambazo zimekuwa zikiwakatisha tamaa wagonjwa.

“Inatakiwa  watumishi katika vituo kujirekebisha na kuzingatia  taratibu za kuadirifu kamavile walivyoelekeza baada ya kuwa wameitimu mafunzo kuwa watafanya kazi kwa uadilifu na pindi wanapofika kwenye vituowamekuwa wakichukua tabia ambazo sio nzuri kwa wateja nah ii ni kutokana na majibu ambayo wamekuwa wakipatiwa wateja sio mazuri”Alisisitiza Kyunga

Pamoja na serikali kusisitiza swala la  watanzania kutumia   bima za afya bado tatizo ni kubwa kutokana na wengi wao kutokuwa na elimu hivyo mamlaka husika zimetakiwa kutoa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa mfuko wa Bima ya afya.



Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.