Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini
ya MOI Prof, Bakari Lembariti akihutubia wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi wa Kikao cha Tatu cha Baraza Hilo, kutoka kulia ni Naibu Katibu Baraza la Wafanyakazi hilo, Mwenyekiti wa Tughe na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa MOI Dkt, Othman Kiloloma
Kaimu Mkurugenzi wa MOI Dkt Othman Kiloloma akiwasilisha ripoti ya Utendaji ya Mwaka 2015/2016,
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa MOI wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Prof, Bakari Lembariti
Makamu mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi MOI Prof , Bakari Lembariti akimkabidhi cheti Mfanyakazi bora wa Taasisi ya MOI kwa Mwaka 2015/2016 Rbert Ojock na pesa TSH. mil. 4(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA). |
KAIMU Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya
MOI Profesa Bakari Lembariti jana amezindua kikao cha Baraza la Tatu la
Wafanyakazi wa MOI katika ukumbi wa IDDI NYUNDO katika halmashauri ya
Temeke jijini Dar es Salaam. kikao kimehudhuriwa na zaidi ya wajumbe 50
kutoka katika kila idara, vitengo na chama cha wafanyakazi wa MOI
(TUGHE) na wajumbe wa TUGHE mkoa.
Akizindua Baraza hilo Profesa, Lembariti
alisema anampongeza Mh, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli, Alisema ” Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini
MOI Mh. Zakia Meghji natumia Fursa hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli kwa uongozi wake uliotukuka
na jitihada zake za kuboresha huduma za afya hapa nchini, sote ni
mashahidi“.
Aidha, Profesa Lembariti aliwakumbusha
wafanyakazi wa MOI kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya
utumishi wa Umma ili kujenga imani kwa watanzania walio wengi ambao
wanaitegemea MOI kama Taasisi pekee inayotoa Tiba ya kiwango cha juu cha
rufaa kwenye Tiba ya Mifupa, upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu.
Pia Profesa, Lembariti alisema ni vyema
wajumbe wa Baraza la MOI wakatumia vikao vya Baraza kujadili changamoto
mbalimbali zinazoikabili Taasisi ya MOI na kutafuta muarobaini ili
Taasisi ya MOI iendelee kutoa huduma bora,
Kwa upande mwingine Profesa, Lembariti
aliwakabidhi zawadi wafanyakazi Bora wa MOI kwa mwaka 2015/2016 ambapo, Robert Ojock na pesa TSH. mil. 4 aliibuka kidedea na kuwa mfanyakazi Bora wa MOI na
kujipatia cheti na fedha taslimu kiasi cha Tshs Milioni 4, nafasi ya
pili ikishikwa na Bwana Lucas Machage akijipatia cheti na kiasi cha Tshs
Milioni 2 na nafasi ya tatu ikishikwa na Bi Betty Shila ambaye
alijipatia cheti na kiasi cha Tshs Milioni 1.5
Kwa upande wake ,akiwasilisha ripoti ya
utendaji wa Taasisi ya Kaimu Mkurugenzi wa MOI Dkt. Othman Kiloloma
alisema kutokana na ongezeko kubwa la ajali ambazo zimepelekea ongezeko
kubwa la wagonjwa MOI, Taasisi ya MOI iko kwenye mpango mkakati kabambe
wa kushirikiana na baadhi ya hospitali za rufaa za pembezoni kwa
kuwapeleka wataalamu kutoa huduma katika hospitali hizo na kupunguza
kama si kuondoa kabisa wimbi la wagonjwa wanaopokelewa MOI.
Dkt, Kiloloma alisema kwamba Taasisi ya
MOI imeendelea kuwa Kitovu cha Weledi katika matibabu ya Mifupa , Ajali
, Ubongo na Mishipa ya Fahamu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na
kati ambapo mwaka 2015 MOI ilitoa utafiti bora wa mfupa mrefu wa paja
duniani ,ambapo utafiti uliwasilishwa katika Taasisi ya kimataifa ya
upasuaji wa mifupa duniani ya Marekani (AOTA)
Vilevile, Dkt. Kiloloma aliwaomba wajumbe
wa Baraza la MOI kutoa michango yenye tija ili kupata matibabu ya
changamoto mbalimbali zinazoikabili Taasisi ili Taasisi iendelee kutoa
huduma bora kwa watanzania
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.