Mwanaharakati Jenerali Ulimwengu naye ameungana na wadau wenzake wa tasnia ya habari mahakamani hapa. |
Na Zephania Mandia
GSENGO BLOG
MWANZA.
Umoja wa klabu ya za Waandishi wa Habari Tanzania UTPC na kampuni ya Hali halisi Publishers Limited leo wamefungua kesi ya katika Mahakama Kuu ya Tanzania Mwanza wakidai kuwa sheria ya huduma ya vyombo vya habari 2016 inakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sheria hiyo ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 5,2016.katika kufungua kesi hiyo,timu ya wanasheria Fulgence Massawe, Edwin Hans, Jenerali Ulimwengu, Jebra Kambole, Frances Stolla, Mpole Mpoki. hawa wote wanaziwakilisha taasisi hizo katika mahakama kuu.
Walalamikaji wanadai kuwa baadhi ya vifungu vya sheria hiyo vinakandamiza uhuru wa kujieleza vinakiuka ibara ya 18 ya katiba ya nchi.
Ibara ya 18 inatoa haki kwa kila mtu kuwa na uhuru wa maoni na fikra zake,kutafuta,kupokea habari bila ya kujali mipaka ya nchi, uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano hayo.
Katiba pia inatoa haki kwakila mwananchi kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu maswaala muhimu kwa jamii.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.