VYA HABARI LEO TAREHE 26.01.2017
·
TAHADHARI
YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA WANANCHI WOTE WA MWANZA NA MAENEO JIRANI
JUU YA UWEPO WA VIKUNDI VYA WAHALIFU WANAOIBIA WANANCHI FEDHA ZAO KWA
KUWASHAWISHI KUJIUNGA NA BIASHARA YA UPATU ( KUWEKEZA FEDHA KIDOGO NA BAADAE
KULIPWA FEDHA NYINGI KWA MUDA MFUPI BILA KUFANYA KAZI YEYOTE) KAMA ILIVYOKUWA DECI .
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MWANZA DCP: AHMED MSANGI ANATOA TAHADHARI KWA WANANCHI WOTE WA MWANZA NA
MAENEO JIRANI KUJIHADHARI/KUJIEPUSHA NA WATU/VIKUNDI VYA WATU AMBAO NI WAHALIFU
WALIOKUSUDIA KUJIPATIA FEDHA NYINGI TOKA KWA WANANCHI KWA KUWADANGANYA/
KUWARUBUNI WAJIUNGE NA BIASHARA YA UPATU AMBAPO WANANCHI HAO HUSHAWISHIWA
KUWEKEZA FEDHA KIDOGO KWA MUDA MFUPI KATIKA VIKUNDI HIVYO NA BAADA YA HAPO
WANAAHIDIWA KULIPWA FEDHA NYINGI ZAIDI YA ZILE WALIZO WEKEZA BILA KUFANYA KAZI
YEYOTE. BIASHARA HIYO INATAMBULIKA KWA JINA LISILO RASMI LA KUPANDA MBEGU NA
KUVUNA.
HIVI KARIBUNI
KUMEJITOKEZA WIMBI KUBWA LA VIKUNDI VYA NAMNA HIYO HAPA JIJI MWANZA NA TAYARI
WANANCHI WENGI WAMEIBIWA FEDHA ZAO. KUTOKANA NA KUONGEZEKA KWA UHALIFU WA AINA
HII JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEANZISHA NA LINAENDELEA NA MISAKO MAENEO
MBALIBALI YA JIJI NA MKOA WA MWANZA, KWA LENGO LA KUBAINI NA KUWAKAMATA
WATU/VIKUNDI VINAVYOFANYA UHALIFU HUO. (UPATU)
AIDHA KAMANDA
ANATAHADHARISHA WANANCHI KUHUSU VIKUNDI VIFUATAVYO AMBAVYO UPELELEZI UMEONESHA
KUWA VINAJIHUSISHA NA BIASHARA YA UPATU AMBAVYO NI; KIKUNDI KINACHOJULIKANA KWA
JINA LA AQ POWER CLUB KINACHOMILIKIWA NA
HAPPY ALOYCE MBUYA MIAKA 35, MCHAGA , MKAZI MTAA WA ILIEMELA ENEO LA
MAHAKAMANI, MFANYABIASHARA NA MKURUGENZI WA KAMPUNI BINAFSI IITWAYO AQ CUMPUTER
CO.LTD, UPELELEZI UMEBAINI KWAMBA MTUHUMIWA TAJWA HAPO JUU AKISHIRIKIANA NA
WENZAKE SABA (7) WAMEFANIKIWA KUKUSANYA FEDHA ZAIDI YA TSH 100,000,000/= KUTOKA
KWA WANANCHI AMBAO WALISHAWISHIWA KUJIUNGA NA KIKUNDI CHAKE, PIA UPELELEZI
UMEBAINI KUWA AQ POWER CLUB SIO TAASISI ILIYOSAJILIWA KISHERI BALI JINA LA
BIASHARA LA MTUHUMIWA.
TAYARI MTUHUMIWA TAJWA
HAPO JUU NA WENZAKE SABA WAMEKAMATWA NA UPELELEZI UNAENDELEA PINDI UKIKAMILIKA
JARADA LITAPELEKWA KWA MWANASHERIA WA SERIKALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA
DHIDI YAO, AIDHA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA ANATAHADHARISHA WANANCHI
KUHUSU SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA KIKUNDI/ KAMPUNI BINAFSI YA BEGA KWA BEGA MICRO
FINANCE COMPANY LTD, KWANI WATU WENGI WAMEKUJA KURIPOTI POLISI JUU YA
KUTAPELIWA FEDHA ZAO NA KAMPUNI HIYO, TAYARI JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA
LIMEWATIA MBARONI WAKURUGENZI NA BAADHI YA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI HIYO NA
MAJALADA YA KESI HIZO YAPO KWA MWANASHERIA WA SERIKALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
AIDHA JESHI LA POLISI
LINAENDELEA KUZIFANYIA KAZI TAARIFA ZA KIINTELEJENSIA KUHUSU TAASISI
ITAMBULIKAYO KWA JINA LA AMKA MWANAMKE (AMWA), KWAMBA PIA INAJIHUSISHA NA
BIASHARA YA UPATU, UCHUNGUZI UNAFANYWA ILI KUWEZA KUBAINI UKWELI WA TAARIFA
HIZO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI
ANAWATAHADHARISHA WANANCHI WOTE WA MWANZA NA MAENEO JIRANI KUJIEPUSHA NA
VIKUNDI VYA AINA HII, PIA ANAWAAASA WANANCHI KUJITAFUTIA KIPATO CHA HALALI KWA
KUFANYA KAZI HALALI NA SIO KUWEKEZA FEDHA KIDOGO (KUPANDA) NA KUTARAJIA KUPATA
FEDHA NYINGI KWA MUDA MFUPI ( MAVUNO). TAMAA YA KUPATA UTAJIRI WA HARAKAHARAKA
UMEWAINGIZA WANANCHI WENGI KWENYE HASARA KUBWA ILIYO TOKANA NA KUIBIWA FEDHA
ZAO KWANI HAKUNA KIKUNDI/ MTU ANAYEWEZA KUPEWA FEDHA KWA MUDA MFUPI ALAFU BAADA
YA MUDA MFUPI ALIPE FEDHA NYINGI ZAIDI. WANANCHI WATAMBUE KUWA HUU NI MTEGO WA
WAHALIFU WA KUWAFANYA WANANCHI WASHAWISHIKE KUJIUNGA NA VIKUNDI HIVYO ILI
WAWAIBIE.
IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M)
MWANZA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.