Kwa sababu hiyo, mahakama hiyo imemhukumu kulipa faini ya Sh 700,000 au kwenda gerezani miaka mitatu.
Murunya aliyekuwa Mhifadhi Mkuu wa NCAA na wenzake watatu, walikuwa wakishitakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 66,890 (Sh milioni 133.7).
Katika kesi hiyo namba 71 ya mwaka 2015, washtakiwa wengine ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa NCAA, Shad Kiambile, aliyekuwa Meneja wa Huduma za Utalii katika mamlaka hiyo.
Wengine ni Veronica Ufunguo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafirishaji wa Anga ya Cosmos Salha Issa, ambao waliachiwa huru na mahakama hiyo baada ya kupatikana hawana hatia.
Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Patricia Kisinda, alisema katika kosa la kwanza ilimtia hatiani Murunya kwa matumizi mabaya ya madaraka.
Hakimu alisema Murunya alishindwa kuithibitishia mahakama kuwa aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, alimwagiza kubadilisha usafiri badala ya kupitia Kampuni ya Cosmos, wasafiri kwa Kampuni ya Antelop Tours.

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.