ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 3, 2016

POLISI YAMTIA MBARONI ASKARI ALIYECHUKUA RUSHWA KUTOKA KWA RAIA WA KIGENI ZANZIBAR.

Jeshi la Polisi Zanzibar limemkamata askari wake anayetuhumiwa kupokea rushwa kutoka kwa raia wa kigeni baada ya kumkamata kwa kosa la barabarani na kumuachia huku akimuahidi kumlinda.
Uamuzi huo wa jeshi la polisi Zanzibar umetolewa na kamishna mkuu wa jeshi hilo hapa Zanziabr CP Hamdan Omar Makame wakati akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya polisi ambapo amesema jeshi la polisi limesikitishwa sana na kulaani kitendo hicho cha askari huyo akipokea rushwa kwa kosa la raia huyo kutovaa mkanda na kitendo hicho kusambazwa kwenye mitandao ambapo amemtaja askari huyo ni sajenti Talib Hamad na siyo jina la Ali huku pia akisema kitendo hicho kilifanyika Mkokotoni na sio Mahonda kama alivyokaririwa askari huyo kwenye mahojiano ya mtandao.
Kamishna mkuu wa jeshi hilo hapa Zanziabr CP Hamdan Omar Makame.
Kamishna mkuu huyo wa polisi Zanzibar amesema kwa sasa askari huyo hatachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu za kipolisi na ikithibitika kuwepo kosa la jinai atapelekwa kwenye vyombo vya sheria vya dola huku na akisisitiza wananchi waendelea kutoa ushirikiano.

Kwa mujibu wa tukio hilo lilivyoonekana kwenye mtandao huo raia huyo alikamtwa kwa kosa la kutovaa mkanda wa gari na askari huyo aliamua kuchukua leseni ya barabara na kumuhakikishia kuwa aendele na safari na atamlinda huku akionekana akipokea fedha taslimu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment