ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 27, 2016

TAZAMA JINSI NORWEGIAN CHURCH AID (NCA) WALIVYO NIGOSHA TAMASHA LA UTAMADUNI HYDOM.

Naibu Balozi Norway   bwana TRYGVE BENDIKSBY .akizindua kisima cha maji kijiji cha ENDAGAW wilayani Mbulu. kutoka kulia ni TALE HUNGNES Mwakilishi Mkazi wa Shirika la NCA Tanzania,Mkuu wa wilaya ya Mbulu Mh.Flatey Massay, Balozi  Msaidizi TRYGVE BENDIKSBY, Bwana Abeli Mfanyakizi wa NCA na Afisa Mradi wa WASH NCA Tanzania Bwana.Zakayo Makobelo.

Bwana Zakayo Makobelo akitoa ufafanuzi Juu ya kisima hiki kitumiacho Nishati ya Jua.
Mbunge wa Jimbo la Mkalama Mh.Allan Kilawa akimtwisha maji mmoja ya wanakijiji wa Munguli wilayani  Mkalama Mkoani Singida.
Mkuu Wa wilaya ya Mkalama Mkoani Singida na Mbunge wa MAkalama wakionyweshwa Vifaa vifaa hivi vya kuzilisha nishati ya jua kwa ajili ya kusaidia Usamabazaji wa maji kijjijni.
Vijana wa YouthCAN wakitoa elimu YA MAZINGIRA,AFYA NA MAJI SALAMA kupitia muziki wakati wa Tamasha la kiutamaduni.
Naibu Balozi wa Norway Tanzania   TRYGVE BENDIKSBY alipotembelea banda la NCA NA 4CCP HYDOM wakati wa Tamasha la Utamaduni Hydom.
Matukio mbali mbali yaliyojiri wakati wa Tamasha la Utamaduni
bwana Girlbert Mwolia Meneja Mradi wa NCA Tanzania na TALE HUNGNES wakizungumza na wananchi wa HYDOM wilayani Mbulu.
Kila mwaka shirika la Four Corner Culture Program (4CCP) huandaa tamasha la kiutamaduni ili kukuza na kuenzi tamaduni halisi za kitanzania .

      Tamasha la mwaka huu limekuwa lakipekee sana kutokana matukio mablimbali ya kimaendeleo na kiutamaduni yaliyofanyika .Ambapo Shirika la Norwegian Church Aid kwa kushirikiana na 4CCP Hydom walizindua  miradi mabli mbali ya maendelea katika sekta ya maji (Visima)ili kupunguza tatizo kubwa la maji linalo wakumba wananchi wa wilayani Mbulu mkoani Manyara na mkoa jirani wa Singida.
PICHA ZOTE NA IMANI NSAMILA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.