ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 26, 2016

NUMET YATOA SIKU 21 KWA SERIKALI(NI KUHUSU FAO LA KUJITOA)

NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza.

 CHAMA cha wafanyakazi wa sekta ya Nishati na Madini Tanzania(NUMET)  kimetoa siku 21 kwa serikali kueleza  muda wa kuanza kutolewa kwa  fao la kujitoa kama ilivyokuwa zamani ikiwemo kurejeshwa kwa mswaada wa fao hilo bungeni.

Chama hicho pia kimeazimia kufanya maandamano nchi nzima  Oktoba 17 mwaka huu endapo serikali itashindwa kutekeleza  mambo hayo mawili  kwa muda walioutoa ili iwe njia ya kuishinikiza kutekeleza kutatua madai yao .

Akizungumza na waandishi wa habari jana Katibu wa chama hicho  Nicomedes Kajungu alisema baada ya maandamano endapo serikali itaamua kuziba masikio na kutokusikiliza kilio hicho,chama kitawataka  waajiri waache kukata michango kwenye mishahara ya wafanyakazi hadi mgogoro  huo utakapokuwa umemalizika.

 “Serikali itambue kuwa wafanyakazi  hawawezi kuweka pesa zao kwenye mifuko ya hiari kwani fedha hiyo wanayoweka haizai faida badala yake inapoteza thamani siku hadi siku hivyo tunahitaji fao hilo liendelee kutolewa kwa sababu waajiri wanachangia kiwango sawa ya kile wanachama wanachochangia ili kuondoa hasara inayosababishwa na kushuka kwa thamaniya shilingi”alisema Kajungu.

Kwa upande wake  katibu wa chama hicho kanda ya ziwa  Shigela  Aloyce alieleza kuwa, serikali ilifanyie mzaha suala hilo kwani hicho ni kipato cha wafanyakazi na kwamba haiungi mkono hoja ya kuweka fedha ili uvune uzeeni kwani hauatkauwa na nguvu ya uzalishaji.

“Watoto wanahitaji kwenda shule  na vijana kufikia ndoto zao iweje utueleze kuipata ela yetu mpaka uzeeni huoni kama tunaongeza kundi la utegemezi  na kushindwa kufikia malengo thamni ya ela ni kidogo na nguvu ya uzalishaji huna tena”alieleza Shigela.

Ikumbukwe kuwa  Serikali  kupitia vikao vyake vya bunge kutaka  kuondoa utaratibu wa fao la kujitoa kupitia mswaada wa sheria ya mifuko ya jamii uliotarajiwa kusomwa kwa mara ya kwanza kwenye bunge  septemba 6 hadi 16 mwaka huu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.