NA VICTOR MASANGU,BAGAMOYO
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Majid Mwanga amekemea na kuvipiga marufuku vitendo vya askari mgambo kuwa na tabia ya kujihusisha na upitishaji wa kuingiza biashara za magendo na badala yake amewataka kuhakikisha wanakuwa wazalendo na nchi yao kwa lengo la kuweza kudumisha hali ya amani na utulivu.
Kauli hiyo imetolewa wakati alipokuwa akizungumza na askari mgambo pamoja na wananchi mara baada ya kumaliza kusherekea maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)ambayo yalikwenda sambamab na zoezi la ufanyaji wa usafi katika mitaa mbali mbali ya Wilayani Bagamoyo ambayo pia yaliwajumuisha wafanyakazi wa ofisi ya mkuu wa Wilaya.
Mwanga alibainisha kwamba askari wanatakiwa kuwafichua wale wote ambao wanajihusisha na biashara hizo,ambazo zimekuwa zikiingia nchini kinyemela kupitia fukwe za bahari ya hindi kinyume na sheria na taratibu na kupelekea kuikosesha serikali kukusanya mapato kama inavyotakiwa kutokana na watu wachache kukwepa kulipa kodi.
“Mbona mnavusha wahamiaji haramu, mbona mnaingiza sukari a magendo,mbona mnashiriki kuvusha tairi za magendo na cha kushangaza hamtuambii lolote, kwa hiyo mimi ninachowaomba tabia hii sio nzuri na kitu kikubwa ni kushirikiana bega kwa began a jeshi la Polisi ii kuweza kuwafichua wale wote ambao wanafanya biashara hizo za magendo,”alisema Mwanga.
Mwanga alisema kwamba kwa sasa wataweka mikakati kabambe kwa ajili ya kuweza kufanya msako wa mara kwa mara katika fukwe za bahari, ili kuweza kuhakikisha kwamba wale ambao wanajihusiha na biashara hizo z amagendo wanakamatwa na wanachukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine.
Katika hatua nyingine Mwanga alisema kwamba katika mkuhakikisha Wilaya ya Bagmoyo inakuwa na mazingira masafi muda wote wameweka faini ya kisi cha shilingi elfu hamsini kwa mtu yoyote atakayebainika anatupa taaka ovyo na kuongeza kuwa kuna program maalumu ambayo itazinduliwa na kushindanisha kata kwa usafi na washindi watapatiwa pikipiki kwa maafisa tarafa na watendaji.
Kwa upande wao baadhi ya askari mgambo akiwemo Frank Mwaisame pamoja na Hamis Ramadhani hawakusita kuelezea changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na kuiomba serikali kuwangalia kwa jicho la tatu katika suala zima la maslahi yao kwani wanafanya kwazi kwa kujitolea.
Nae Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Erica Yegella mewaasa wakinamama wanatumia fursa zilizopo kwa ajili ya kuweza kuleta chachu ya maendeleo pamoja na kuwaasa kufanya usafi katika maeneo yao ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.
Reha Mita ni Kaimu mshauri wa mgambo Wilaya ya Bagamoyo pamoja na Mkuu wa jeshi la polisi Wilaya ya Bagagamoyo Adam Maro ambaye ni mkuu wa jeshi la Polisi Wilaya ya Bagamoyo walisema askari wanapaswa kuwa wazalendo na nchi yao ili kudumusha amani iliyopo. na hapa walikuwa na haya ya kusema kuhusiana na maadhimisho hayo.
KATIKA kusherekea maadhimisho hayo ya miaka 52 ya Jeshi la wananzhi wa Tanzania (JWTZ) Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo ameongoza zoezi la kufanya usafi kwa kuamaua kuendesha mwenyewe gari la kubebea takataka na kupita katika mitaa mbali mbali jambo ambalo liliweza kuwa ni kivutia kikubwa kwa wananachi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.