NA VICTOR MASANGU, RUFIJI
MBUNGE wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa katika kuunga juhudi za serikali katika kuboresha viwanja vya mpira ametoa msaada wa mabati 650 kwa ajili ya kuweza kuweka uzio ambao utaweza kusaidia kuingiza ukusanyaji wa mapato pamoja na kukuza na kuviendeleza vipaji vya mchezo wa soka kwa vijana.
Akikabidhi msaada huo wa mabati 650 katika hafla iliyofanyika katika uwanja huo wa mpira wa shule ya msingi Muhuro Mchengerwa aliesema kwamba uwanja huo umekuwa ukitumika katika mashindano mbali mbali lakini changamoto kubwa ilikuwa hakuna uzio.
Mchengerwa alionngeza kuwa lengo lake kubwa ni kuona katika jimbo lake vijana wote wanashiriki kikamilifu katika michezo ili kuweza kupata wachezaji wenye vipaji ambao wataweza kuchezea hata timu ya Tiafa katika siku zijazo.
“Mimi kama mbunge a jimbo la Rufiji nia yangu kubwa ni kuhakikisha kwamba ninawekamikakakti kabambe ya kuwaendeleza vijana katika suala zima la michezo, na ndio maana nimeona kuna umhumihu mkubwa katika uwanja huu kuuzungushia uzio wa mabati, ili pindi ligi mbali mbali zinapofanyika kuweze kuwa na kiingilio ili fedha zitakazopatikaka ziweze kusukumu gurudumu ya kuendeleza michezo,”alisema Mchengerwa.
Aidha alibainisha kwamba wakati alipokuwa katika mchakato wa kampeni zake aliwaweza kuahidi kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya michezo kuanzia ngazi zote z vijiji hata ngazi ya Wilaya ikiwemo sambamba na kuboresha viwanja ambavyo vipo katika jimbo lake la Rufiji.
Pia alisema katika ktimiza azma yake ya kufufua vipaji kwa vijana na kuviendeleza endeleza anatarajia kuanzisha mashindano makubwa ya mchezo wa soka ambayo yatazishirikisha timu mbali mbali kutoka kata zote 13 zilizopo katika jimbo lake.
Katika hatua nyingine Mchengerwa aliomba Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kuweka utaratibu wa kwenda kutembelea timu zilizopo katika maeneo ya vijijina kwani kuna vijapi vingi ambavyo vinashindwa kuonekana kutokana na kutokupata sapoti ya kutosha hivyo kusababisha kukokosa wachezaji wazuri ambao wanatokea ngazi za chini.
“Hapa kwa hili pamoja na kuendeleza na juhudi za ngungu za kuendeleza vijaji vya wachezaji lakini TFF, ambao ndio wasimamizi wa mchezo huu wa soka kulianagalia suala hili kwa jicho la tatu, hususan kwa upande wa wachezaji wa ngazi za chini, kwani mimi nimeweza kubaini kuna wachezaji wengi wazuri sana ila changamoto wanajikuta wanakosa sapoti na kuwepo kw achangamoto ya viwanja,”alisema Mchengerwa.
Katika hatua nyingine aliongeza kwamba katika kukuza sekta ya michezo atahakikisha kwamba kwa sasa anaweka program maalumu kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa mchezo wa soka ili kuweza kuwasaidia wachezaji wenye vipaji, sambamba na kuwapatia vifaa mbali mbali kwa ajili ya kuwasaidia waweze kufanya mazoezi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.