ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 28, 2016

ALIYEPIGA PICHA YA DAUD MWANGOSI AKIUAWA JOSEPH SENGA, AFARIKI DUNIA(4)

Enzi za uhai wake.
Joseph Senga mpiga picha wa Gazeti la Tanzania Daima amefariki usiku wa kuamkia leo nchini India alikuwa akitibiwa.

Senga ndiye aliyepiga picha ya Mwangosi akiwa amezingirwa na polisi alipopigwa Bomu na kuuawa,  hukumu imetoka jana.
R.I.P Senga.

Ameandika dotto Simanzi,siku moja baada ya mahakama kuu kanda ya Iringa kumfunga miaka kumi na mitano askari ya aliyemuua Daudi Mwangosi,tasnia ya habari yapata pigo, mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima, aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Daudi ya Mwangosi, SHUJAA JOSEPH SENGA, amefariki dunia usiku wakuamkia leo .
Senga amefia nchini India alikopelekwa kwa matibabu ya ugonjwa wa Moyo.
Bila Joseph Senga, shujaa aliyehatarisha maisha yake, akasimama bila woga, akapiga picha akiwa katikati ya msitu wa askari polisi wenye silaha, huku anga ikiwa imegubikwa na moshi wa mabomu ya machozi, milio ya risasi ikisikika, na kuzitunza, zikasaidia kufichua mauaji ya Mwangosi, leo hii asingekuwa Senga,nadhani kusingekuwa na kesi na mwisho hukumu dhidi ya aliyemuua Mwangosi.
Nakulilia Senga.. Senga, Senga, Senga, Senga, umekwenda, Mungu aliamua akuweke hai mpaka hukumu itoke na mwisho amekuchukua, Senga umekwenda wadogo zako katika tasnia tukiwa na hamu ya kujifunza kutoka kwako.
Senga,Senga,kamsalimie Daudi Mwangosi,mwabie aliyemuua nae kahukumiwa jela miaka 15,kamwambie mazingira ya waandishi wa habari bado magumu.
Nenda Senga, picha zako zinabaki kuwa rejea ya mafunzo ya uandishi wa habari katika mazingira hatarishi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.