Katika mjada ulio wasilishwa, wadau wameishauri serikali kupia Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEC, kuboresha sheria ya usimamizi wa mazingira ili kuweza kuwafanyia tathmini za uchafunzi wa mazingira wachimbaji wadogo kwa kuwa baadhi yao wamekuwa wakichangia uchafunzi wa mazingira nchini.
Kwa umakini na kumbukumbu daftarini, wadau wa mazingira wakichukuwa pointi. |
Kasi ya maendeleo katika nchi zinazoendelea inaweza kurudi nyuma miaka mitano ijayo,iwapo hatua thabiti hazitachukuliwa kupunguza kasi ya uharibifu wa mazingira.
Ripoti ya 2011 kuhusu uendelevu na usawa ilieleza kuwa, uendelevu wa mazingira unaweza kufikiwa kwa njia ya haki na yenye matokeo mema iwapo masuala ya afya, elimu, kipato, na tofauti za jinsia kuchukuliwa hatua za kimataifa kuhusu uzalishaji wa nishati na utunzaji wa mazingira.
Uharibifu wa mazingira unatishia uhai wa viumbe duniani kwa kiasi kikubwa kutokana na shughuli mbalimbali za wanadamu ikiwemo ukataji miti na uchomaji moto misitu ya asili.
Msisitizo mkubwa umekuwa ukifanywa na wadau wa mazingira kwa kuhakikisha mikataba na sheria zinawekwa ili kulinda, mazingira na viumbe adimu wasitoweke.
Tanzania ni moja ya nchi duniani zilizobarikiwa kuwa na misitu ya asili na mito mikubwa isiyokauka maji kwa kipindi cha mwaka mzima.
Mbali na vivutio hivyo,kumekuwa na uelewa mdogo wa masuala ya uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji miongoni mwa jamii.
Ukosefu wa elimu kwa jamii ya Watanzania umesababisha wananchi kushindwa kutambua umuhimu wa kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji vilivyowazunguka katika maeneo yao.
Wadau wa habari ambao vile vile ni Bloggers wa Mwanza, kutoka kushoto Gsengo, Atley Kuni na Kijukuu cha Bibi. |
Mchanganuo toka katika jedwali la Makampuni na kuanzishwa kwake ikiwa ni pamoja na mapitio ya sheria ya mazingira. |
Wadau wa mazingira wamekusanyika hapa |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.