Airtel yaendelea kuwapatia watanzania simu zenye uhalisi.
• Simu za Bure katika maduka ya Airtel nchi nzima
• Vifurushi vinavyodumu kwa miezi minne na dakika zaidi ya 1000
Dar Es Salaam, 16 Juni 2016, Kufuatia tamko la serikali la kuzima simu zote bandia ifikapo tarehe 16 Juni 2016, Airtel Tanzania imeendelea kutoa ofa kabambe za “simu za bure na halisi" zinazopatikana katika maduka yote ya Airtel nchi nzima. Tangazo hilo limesema kwamba simu za Bure na halisi zinapataikana kwa wateja wote wenye simu bandia na ambazo sio za viwango vinavyokubalika katika soko la Tanzania , kwa kununua kifurushi chenye dhamani ya sh. 22,000 / = Tshs tu. Simu hizi za bure na halisi zinazotolewa na Airtel ikiwemo ITEL 2090 na FERO 180, zikiwa na dakika 550 kwa kupiga mitandao yote, zenye ujumbe mfupi 3000 na 250 MB kwa muda wa miezi minne.
Akitoa maoni yake juu ya ofa hii, mkuu wa kitengo cha Internet Airtel Tanzania, Gaurav Dhingra alisema "kwakutambua kwamba baadhi ya wateja wetu bado wanatumia simu ambazo hazina uhalisia, tumeendelea kufanya jitihada za kuwapatia simu halisi.Napenda kusisitiza kuanzia kesho kwa wale wenye simu zitakazo zima leo usiku wasi hofu kwani laini zao hazitahadhirika na vifurushi na pesa ndani ya simu zao zitaweza kutumika pale watakapo nunua simu zenye kiwango kinachokubalika kwenye maduka yetu nchi nzima kwa kupata simu halisi, na vifurushi vitakavyo dumu kwa miezi mine
Le tupo maeneo ya mnazi mmoja katika ofisi za halmashauri ya manispaa ya Ilala, ambapo wiki ijayo wataendelea kuwepo katika ofisa za halmashauri ya manispaa ya Ilala na Kinondoni. Dhingra aliendelea kufafanua kuwa, ili kuwapa wateja wetu uwezo wa kuchagua simu zinazokidhi mahitaji yao ,tumeongeza simu za aina mbalimbali ikiwemo Magnus Z11, Huawei Y3C na Techno W3 ambapo mteja akinunua anapata kifurushi chenye dakika zaidi ya 1000 . "Tunatoa wito kwa wateja wetu wa Airtel wenye simu bandia kufika kwenye duka letu lolote la Airtel na simu yake ili ajipatie simu yenye kiwango kinachokubalika kwa gharama nafuu zaidi kwa kununua kifurushi cha Airtel na kupata simu bure. "alinukuliwa Dhingra
Wateja wa Airtel wanaweza kuhakikisha kama simu zao ni bandia au la, kwa kupiga *#06# au kutembelea mawakala katika maduka ya Airtel lililokaribu nae.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.