mwenyekiti wa CCM kata ya Sakina Neema Molel ambaye pia ni mwaandaaji wa tamasha la vijana akiwa anasalimiana na wachezaji wa moja ya timu ambazo zimeshiriki tamasha hilo
Alikuwa mgombea ubunge wa viti maalumu wazazi kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi ,ambaye pia ni mkurugenizi wa Phideintatament Phidesia Mwakitalima akiwa anasalimiana na timu kabla ya mechi za siku hiyo kuanza
muandaaji wa mashindano hayo wa kwanza kulia Neema molel akifuatana na mkufunzi ambaye ni mkurungezi wa kituo cha kukuza vipaji vya vijana (Rolling stone)Ally Mtumwa tayari kwa kukagua timu kabla ya mechi kuanza
naye muimbaji wa nyimbo za injili
Neema Kasambale nae pia aliudhuria kuangalia jinsi vijana wanavyo
sakata kabumbu
mwenyekiti wa CCM kata ya Sakina Neema
Molel ambaye pia ni mwaandaaji wa tamasha la vijana akiwa
anasalimiana na wachezaji wa moja ya timu ambazo zimeshiriki tamasha
hilo
wachezaji wakiendelea kusakata kandanda
ndani ya kiwanja cha ngarenaro mkoani
arusha
mashabiki pia waliudhuria kuangalia baadhi ya mechi
Na Woinde
Shizza,Arusha
vijana wametakiwa kujijengea tabia ya
kushiriki michezo mbalimbali kila mara badala ya kujiingiza katika
makundi mabaya ya wizi pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevya kitu
ambacho kinawaaribia mfumo mzima wa maisha
yao.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa
CCM kata ya Sakina Neema Molel ambaye pia ni mwandaaji wa
Tamasha vijana la mpira wa miguuu linaloendeshwa kwa mfumo wa ligi ya
mpira wa miguu linayowashirikisha vijana kutoka katika kata ya sakina
.
Alisema kuwa yeye kama mama anaumia sana
kuona vijana wanakaa mitaani na kujiingiza katika vitendo mbalimbali
mbali ikiwemo wizi pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevywa ivyo
ameamua kuanzisha ligi hii ili kuwasaidia vijana wengi kushiriki na
kuachana na makundi .
"unajua pia michezo ni ajira hivyo nimeona
ni vyema mimi kama mama kiongozi wa watoto nianzishe ligi hii ya
mpira wa miguu ili awa vijana wetu waweze kushiriki,kujifunza na pia
ule mda walikuwa wanatumia kwenda kuangaika uko mtaani na kutumia
madawa ya kulevywa watakuja apa watashiriki michezo "alisema
Neema
Aidha alibainisha kuwa ligi hii aitaishia
kipindi hichi kwani itakuwa endelevu na ameamua kuanza na watoto wa
kiume kwa kuanzisha mpira wa miguu lakini pia anania yakuanzisha ligi
ya wanawake ya mpira wa pete ili pia kuwawezesha watoto wakike nao
kujitokeza na kujifunza kwani michezo pia ni ajara pamoja na
afya.
Kwa upande wake Aliekuwa mgombea wenyekiti
wa CCM mkoa wa Arusha ambaye alikuwa mgeni rasmi katika siku hii ya
uzinduzi wa mashindano hayo Emanuel Makongoro alisema kuwa
amefurahishwa sana kuona jinsi vijana walivyojitokeza kushiriki ligi
hiii kwani wametambua umuimu wa michezo katika afya
zao.
Aliwasihi vijana kuachana nakujishulisha na
biashara za madawa ya kulevya pamoja na unywaji wa pombe za
makaratasi(viroba) badala yake washiriki katika michezo mbalimbali na
hata kama amna ligi basi washiriki katika mazoezi kwani wakifanya
mazoezi yanaweza kuwasaidia kuondokana na vishawishi mbalimbali
vinavyoweza kuwapata .
Kwa upande wa aliyekuwa mgombea ubunge viti
maalumu wa wazazi CCM mkoa wa Arusha Phidesia Mwakitalima alisema kuwa
timu hizo bado zinakabiliwa na changamoto nyingi hivyo wanaitaji
wadhamini na wafadhili wakubwa kujitokeza ili kuweza kunyanyua vipaji
vya vijana hao wa Kata ya sakina pamoja na Kata zote za mkoa wa
Arusha
Aidha alisema kuwa wakiwawajenga vijana katika
michezo itasaidia kupunguza makundi mabaya mitaani na kupelekea
vijana kujituma.
Ligi hii ya Tamasha la vijana wa Sakina limeanza rasmi mapema
mwanzoni mwa mwezi huu na inatarajiwa kumalizika jumapili ambapo
mshindi atapatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo makombe ,jezi pamoja na
mipira .
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.