Mratibu wa Asasi ya kuinua maendeleo ya
Jamii na Kuhifadhi Mazingira (Ececo)Ndosho Hamisi akisisitiza jambo
wakati akitoa mada juu ya madhara ya rushwa ya ngono iliyofanyika kijiji
cha Duga wilayani Mkinga iliyokuwa na lengo la kuwapa uelewa jamii ya
wasichana wa wafuigaji wa kimasaia iliyofanyika
Baadhi ya wananchi wa Kata
ya Duga Maforoni wakifuatilia mada mbalimbalio zilizokuwa
zikiwasilishwa
Katibu wa Asasi ya Kuinua Jamii na
Kuhifadhi Mazingira (ECECO TANZANIA),Said Kamba akisisitiza jambo kwa
washiriki wa semina hiyo
Diwani wa Kata ya Duga
Maforoni Ally Ally akizungumza katika semina hiyo
IMEELEZWA kuwa rushwa ya ngono
imekuwa ni tishio hapa nchini hali inayochangia kurudisha nyuma kasi ya
maendeleo kwani imekuwa ikipunguza demokrasia na utawala bora kwa
watanzania jambo ambalo linapaswa kupigwa vita kwa vitendo.
Hayo
yalisemwa juzi na Mratibu wa Asasi ya Kuinua Maendeleo ya Jamii na
Kuhifadhi Mazingira (Ececo), Ndosho Hamisi wakati wa semina ya rushwa ya
ngono iliyofanyika Kijiji cha Maforoni Kata ya Duga wilayani hapa na
kufadhiliwa na Women Fund Tanzania (WTF)iliyokuwa na lengo la kuwapa
uelewa juu mambo hayo kwa wasichana na wanawake hasa wa jamii ya
wafugaji wa kimasai.
Alisema
kuwa tatizo hilo limekuwa likichukua kasi kwenye sekta nyingi na
kusababisha kukandamiza haki za wanaostahili kuweza kupata fursa za
kuweza kupata nafasi za kukuza uchumi wao na hivyo wengi wao kuishia
katika hali duni.
“Ukiangalia leo hii unaweza kutaka kitu Fulani mahali lakini kwa sababu
hauna sifa ambazo zinapaswa kukipata basi yanaweza kutumika mazingira
ambayo sio sahihi ili uweze kukipata kutokana na kumtimizia mahitaji
yake mlengwa na hili limekuwa tatizo kubwa “Alisema.
“Ni
kosa kisheria mtu mwenye mamlaka kumpandisha cheo mfanyakazi wake
kutokana na kuwepo kwa mazingira ya rushwa ya ngono kwa sababu
inasababisha kupunguza ufanisi kazini na hivyo kushindwa kupiga hatua
kubwa za kimaendeleo “Alisema.
Alisema
jambo hilo limekuwa na madhara mengi kwa jamii ikiwemo kupata magonjwa
makubwa ikiwemo ukimwi lakini pia uzalilishaji kitendo ambacho
kinapelekea kushusha utendaji na kuchangia kurudisha nyuma
maendeleo.
Awali
akizungumza wakati akifungua semina hiyo, Diwani wa Kata ya Duga, Ally
Mohamed aliipongeza asasi hiyo kwa kuona umuhimu kuwapatia mafunzo hayo
ambayo yataweza kuwapa uelewa juu ya madhara ya rushwa ya ngono na
kubadilika
“Unaweza
kukuta wakati mwengine watoto wadogo wanazalilika kutokana na kutokujua
madhara ya rushwa ya ngono hivyo semina hii itawafungua macho kuona
namna ya kuweza kupiga vita vitendo hivyo “Alisema
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.