Polisi nchini India wanasema kuwa zaidi ya watu 100 wameuawa na wengine 150 kujeruhiwa katika moto uliotokea katika hekalu la Wahindu katika jimbo la Kusini la Kerala.
Moto huo uliotokea katika wilaya ya Kollam ulianza wakati wa sherehe ya mapema asubuhi.
Waziri wa mashauri ya nchini katika jimbo la Kerala, Ramesh Chentallah, alisema kuwa uchunguzi wa mahakama utaanzishwa.
Polisi wanasema huenda moto huo ulianzishwa na fataki. |
Polisi wamesema kuwa moto huo umedhibitiwa lakini shughuli za uokozi zingali zinaendelea.
Uchunguzi wa kwanza umebaini kuwa maafisa wakuu katika eneo hilo waliwanyima waratibu wa maonesho hayo leseni ya kuandaa maonesho ya fataki kufuatia hofu kuhusu usalama wa umma.
Waziri mkuu wa India bwana Narendra Modi amewasili Kerala.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.