ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 11, 2016

ALICHO KISEMA DOGO RICHIE KUHUSU MUZIKI WAKE NA BARAKA DA PRINCE

Moja kati ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya wenye muziki mzuri ni pamoja na Dogo Richie a.k.a "Richie Ree" ingawa bado kunawatu hawaja mtambua vizuri muziki wake.

 Baada ya kuisikiliza na kuitazama video ya wimbo wake mpya "Yoyoba" na kupitia nyimbo zake kadhaa Super News Tz team iliamua kumfuatilia na kutaka kujua life style yake ya Muziki ipoje, baada ya kumpata msanii huyo alilazimika kufunguka na kusema.

 “Kwa majina naitwa Francis Kazungu Kalama Jina la sanaa Dogo Richie a.ka Richie Ree, Baba yangu ni Mkenya Mama yangu ni Mtanzania mimi ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya watoto 6, nilianza muziki 2013 Studio yangu ya kwanza kuingia ilikuwa ni ‘Jungle Masters’ chini ya Producer ‘Emmy D’ ambaye ndiye Producer wangu hadi sasa.

 Hadi kufikia sasa nina jumla ya nyimbo 4 na Collabo moja Naona raha, Sina raha, Yoyobah, Hayana Mjuzi & So nice ft. Sam Wa Ukweli. 

‘Naona raha’ ni moja kati nyimbo zilizo nitambulisha vizuri, Muziki katika maisha yangu ndio kila kitu no muziki hakuna kinachoweza kwenda ingawa kupitia muziki nimeweza kuanzisha biashara zangu ndogo ndogo ambazo pindi napo kuwa sina Show zinakuwa zinanisaidia kuendesha maisha.

Baraka Da Prince ni msanii ninaye mfagilia sana Tanzania, coz anamuziki mzuri, Changamoto kwenye muziki zipo ila kikubwa ambacho nakiona kwangu ni ‘Marketing’ ya muziki wangu ili uweze kufika mbali zaidi, coz malengo yangu ni makubwa yaani ni kufika level za kimataifa.

Mwisho nimshuru mwenyezi Mungu, Fans wangu na wadau wote wanao endelea kunipa support kwenye Muziki maana wao ndio maisha yangu Thanks”.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.