Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Conrad Mselle akimfanyia usafi wa nywele mmoja wa watoto wanao lelewa katika Kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi waliopo Buhangija Mkoani shinyanga walipofika katika kituo hicho kwa mwendelezo wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno ambapo kilele chake ni Machi 20, Mkoani Morogoro. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA, MKOANI SHINYANGA, BUHANGIJA)
Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Conrad
Mselle akimfanyia uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno Mwanafunzi wa Darasa
la pili Lucia Eliasi wa Kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi kilichopo Mkoani Shinyanga, Buhangija ambapo ni mwendelezo wa wiki
ya kinywa na meno duniani na kwa leo wameonwa watoto157 na kesho ni mwendelezo wawale waliokutwa na matatizo.
Daktaribingwa wa Afya ya Kinywa na Meno Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga
Dk. Nuru Mpuya na akimwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk.
Ntuli Kapologwe, akizungumza jambo, kushoto ni Kiongozi wa Msafara Dk. Arnold Mtenga
msimamizi wa Kituo cha Buhangija na Mwalimu wa Elimu Maalum na watoto wasioona, Sasu Nyanga , akiwakaribisha Madaktari bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno
Daktari Bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno wa Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Kituo hicho kwa Mapokezi na uongozi huo kuboresha mambo waliyoyaomba mwaka jana yametekelezeka, mfano,kuwekewa kituo cha afya ya kinywa na meno eneo hilo.
Mhudunu wa Afya Mwandamizi, Scolastica Sawaki (kushoto) akimpatia Dawa ya kujipata Esther Gada (kulia) mara alipofika katika Zahanati iliyopo kituoni hapo , ambapo mwanafunzi huyo amefadhikiwa na Claire Grubbs kutoka America na kufadhili mambo mengi shuleni hapo kwa kusomesha baadhi ya watoto Veta wengine kwa lengo la kujifunza , Kutengeneza Batic, ufundi wa Cherehani, utengenezaji wa sabuni, anaye shuhudia ni Mhudunu wa Afya Mwandamizi wa kituoni hapo, Felister Jagadi
kiongozi wa msafara kutoka katika hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Arnold Mtenga, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akiushukuru uongozi wa kituo hicho kwa mambo muhimu waliyoyaomba yafanyike na uongozi wa kituo umeteketeza na kuzidi kuwaomba mara wanapo hitaji msaada kwa watoto haoa wasisite kutoa taarifa na wameonwa watoto 157
Baadhi wa watoto wakimlilia Mmoja wa Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.