Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Conrad Mselle akizungumza na watoto wanao lelewa katika kituo cha watu wenye ulemavu wa ngozi Buhangija mapema leo asubuhi alipokuwa akiwapa Elimu ya upigaji mswaki na utunzaji wa kinywa kwa ujumla na utunzaji wa miswaki yao mara wamalizapo kupiga mswaki na kuwaomba japo kupiga marambili kwa siku (POCHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Conrad Mselle, akiwatolea mfano kwa Mmoja wa watoto hao
Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili, Germana Vincent akigawa flana kwa mtoto mwenye ulemavu wa macho wanao lelewa katika kituo cha Buhangija
Watoto wenye ulemavu wa ngozi wanao lelewa katika kituo cha Buhangija Mkoani Shinyanga wakiimba nyimbo ya kuwaombea Dua Madaktari hao wakiwa wameinua mikono yao juu
Baadhi ya Timu ya wasaidizi wa Kituo hicho cha watoto wenye ulemavu wa ngozi akiwemo Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Conrad Mselle, (wa pili kulia)
Kiongozi wa Msafara ambaye pia ni Daktari wa Afya na Kinywa na meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Arnold Mtenga (katikati) akiteta jambo na madaktari wenzake, kulia ni Conrad Mselle na kushoto ni Germana Vincent, wote kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili
Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno, Sr, Benjamini Buya (kulia) wa Hospitali ya Huruma DDH yaWilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro akitoa elimu ya Afya ya Kinywa na Meno kwa Walezi na Wasimamizi wa Kituo hicho
Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Conrad Mselle akimweka ganzi kwa lengo la kumg'oa meno mawili ya mbele
Profesa
Lembariti akimwelekeza mwanafunzi wa kituo hicho cha Buhangija kwa matumizi ya mswaki na kutunza Afya ya Kinywa na Meno huku wanafunzi wengine wakiangalia kwa makini
Daktari bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga
Dk. Nuru Mpuya (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja kwenye chumba cha Ofisi ya Hospitali hiyo na madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, kulia ni Mmiliki wa ujijirahaa blog, Kamisi Mussa
Profesa
Lembariti akizungumza na Mtoto Suzy Aseng (8), wa Shule ya Rittle Treasures ya Bungayambelele Darasa la 4, alipokuja katika kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi Buhangija mara aliposikia kuwa kunamadaktari wa Afya ya Kinywa na Mane watakua wakitoa huduma ya Afya ya Kinywa na Meno na ndipo alipompa Elimu ya kuhusiana na upigaji mswaki na kumuelekeza mara akiona mswaki unaanza kupinda amwambie mlezi ambadilishie mswaki
Daktari Wa Fya ya Kinywa na Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili Dr. Germana Vincent (kushoto) akizungumza jambo na Madaktari wenzake wakati walipotembelea Kituo cha Watoto wenye ulemavy wa ngozi wa Kituo cha Buhangija Mkoani Shinyanga ikiwa ni mwendelezo wa Wiki ya Afya na Kinywa na Meno ambapo kilele cha Maadhimisho hayo yatafanyika Kitaifa Mkoani Morogoro Machi 20, 2016, kuanzia kulia ni Dr, Gustav Rwekaza wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Daktari bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga
Dk. Nuru Mpuya na Dr, Gerald George wa Hospitali ya Jiji la Tanga
Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno Hospitali ya Manispaa ya Kinondoni Dr. Iddi Khery akimuhudumia Mmoja wa Mwanafunzi wa kituo cha Buhangija
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.