ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 17, 2016

RUSHWA YAWANG'OA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI 4

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anaye shughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nchini Tanzania TAMISEMI Mhe. George Simbachawene ame wasimamisha kazi wakurugenzi wa Halmashari nne nchini kwa tuhumiwa za kutoa rushwa kwa maofisa wa ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ili kubatilisha hati chafu zilipata halmashauri zao. 

Wakurugenzi hao ni wa Halmashauri ya Manispaa ya Misenyi Kagera Elizabeth Kitundu, Halmashauri ya Nanyumbu Mtwara Mohamed Kesenge, wa Halmashauri ya Kilolo Iringa Luckson Pila na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita Abdalla Mfaume. 

Wakati huo huo Simbachawene amemvua madaraka mkurugezi wa mji wa Tunduma Halima Mpita na kuagiza mamlaka zimsimamishe kazi kupisha uchunguzi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka ikiwa ni pamoja na kuwatumia watoto wake katika shuguli za halmashauri na kuwalipa posho na kusababisha upotevu wa mapato

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.