Mkuu wa wilaya ya Busega Paul Mzindakaya akiwakilisha changamoto za wilaya yake kwa waziri mbarawa |
Waziri mbarawa akisikiliza ripoti kwa mkuu wa wilaya ya busega Paul Mzindakaya |
Na Shushu Joel,Busega.
HALAMASHAURI ya wilaya ya Busega nkoani Simiyu imeagizwa kuanza mara moja kutumia mfumo wa kietroniki kuanzia sasa kwa ajili ya kuimalisha mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa ajili ya utoaji wa huduma safi kwa jamii.
Agizo hilo limetolewa jana na Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano nchini Makame Mbarawa wakati alipokuwa anakagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.
Mbarawa alisema kuwa mfumo huo utawasaidia katika kurahisisha kazi mbalimbali na pia utaongeza mapato ya serikali na kupunguza wizi unaotokana na matumizi mabaya ya hundi ambao umekuwa ukiinyima serikali kipata cha kutosha na hii ni kutokana na hata watumishi wa serikali kutokuwa na uaminifu wa kutosha sasa naagiza kuwa kufikia mwanzoni mwa mwezi wa tatu muanze kutumia mfumo huo.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halamshauri hiyo Gaudencia Bamugileki amesema kuwa watahakikisha wanatekeleza agizo hilo la waziri ndani ya mwezi huu ili kuondoa changamoto zilizopo kwa wanajamii.
Alipongeza kuwa mfumo huu pia ni mzuri sana katika ukusanyaji wa mapato na hata kutaifanya halmashauri yangu kupaa kimaendeleo kwani tutakusanya mapato mengi na hivyo kuweza kupiga hatua kubwa katika maendeleo na kufanya wilaya hiyo kuwa ni ya mfano wa kuigwa ndani ya nchi hii alisema.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Paul Mzindakaya amempongeza waziri mbarawa na kuweza kumhakikishia kuwa mashine hizo zitapatikana ndani ya mwezi huu na kuanza kazi kama kawaida ili ziweze kuiongezea kipata serikali yetu kwa ujumla.
Pia mzindakaya aliongeza kuwa mashine hizo zikija inapaswa kutumika vizuri kwani watu wamekuwa na akili mbaya za kuchakachuo mashine hizo hivyo kwa wale watakao bainika kufanya hivyo wajiandaa kuachishwa kazi .
Aidha mkuu huyo wa wilaya alimpongeza waziri mbarawa kwa jitihada zake katika shughuli za maendeleo na kumuomba asichoke kuwasaidia wanabusega katika maendeleo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.