Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Michael Dennis Mhina ‘John Woka’ Hatunaye tena.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kwa staili yake ya kuimba kama mlevi, Michael Dennis Mhina ‘Joni Woka’ amefariki dunia alfajiri ya leo.
TAARIFA ZA AWALI
Akiongea kwa simu kaka wa marehemu Omari Milay, amesema walipigiwa simu alfajiri ya leo na kujulishwa kuwa Joni Woka amefariki katika hospitali ya Muhimbili, alipokuwa akipata matibabu ya ajali aliyopata siku ya jana.

Joni Woka alipata ajali ya kugongwa na kitu kizito kwenye paji la uso, alipokuwa garage maeneo ya Sinza akitengeneza gari yake, kwa bahati mbaya mtungi wa gesi ukalipuka na moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani.
Tarifa za awali za madaktari zilisema wanahofia kipande hiko kimefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.
MIPANGO YA MAZISHI
Baba wa marehemu anasema kuwa Mipango ya mazishi inafanyika Ilala jijini Dar es salaam na mazishi yatafanyika mkoani Tanga ZAIDI BOFYA PLAY KUMSIKILIZA BABA WA MAREHEMU.
Baba wa marehemu anasema kuwa Mipango ya mazishi inafanyika Ilala jijini Dar es salaam na mazishi yatafanyika mkoani Tanga ZAIDI BOFYA PLAY KUMSIKILIZA BABA WA MAREHEMU.
Msanii John Woka ambaye alikuwa kwenye kundi la Watukutu Family, alijipatia umaarufu kwa nyimbo zake za Sophia, baby gal na nyinginezo, ambazo aliziimba kwa mtindo wa ulevi.
Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu. Amen.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.