Papa Francis. |
CHANZO: BBC SWAHILI
Mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa wazo la mgombea wa kiti wa chama cha Republican nchini Marekani , Donald Trump la kujenga ukuta kati ya Mexico na Marekani si ukristo.
Papa Francis alisema kuwa kwa mtu yeyote ambaye katika karne hii ya 21 anayetaka kujenga ukuta badala ya kujenga daraja huyo si mkristo
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki aliyasema hayo katika siku yake ya mwisho ya ziara nchini Mexico.
Trump ambaye anapigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Republicans katika uchaguzi mkuu ujao amependekeza kujenga ukuta na ua katika mpaka kati ya nchi yake na mexico ilikuwazuia wahamiaji kuingia nchini Marekani.
Trump amesema kuwa Papa Francis hana haki yoyote kumhukumu iwapo ni muumini au la. |
Licha ya kuwaambia waumini wa kanisa Katoliki kuwa hatawazuia kutumia uhuru wao kumchagua rais wanaompenda, papa Francis amesema kuwa iwapo Trump anapanga kujega ua basi ''si mkristo''
Hilo haliambatani na mafunzo ya injili
"sharti tutathmini matamshi yake '' tunapaswa kuchunguza kwa kina ''
Bwenyenye Donald Trump kwa upande wake amesema kuwa papa Francis hana haki yeyote kumhukumu iwapo ni muumini au la ''inasikitisha'' alisema Trump.
Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki aliyasema hayo katika siku yake ya mwisho ya ziara nchini Mexico. |
Mtazamo huo wa papa Francis bila shaka unatarajia kuwapa wapinzani wa Trump fataki huku wakiendelea na kura za mchujo ambapo msimamo wa kidini wa mgombea unatazamwa na wapiga kura wengi kuwa kigezo muhimu.
1 kati ya wamarekani 5 ni wakatoliki.
Papa Francis ni maarufu sana nchini Marekani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.