Viongozi wa ligi ya Uingereza
Leicester wamewashangaza wapinzani wao wa karibu katika ligi hiyo
Manchester City baada ya kuwacharaza 3-1 katika uwanja wa Etihad na
hivyobasi kupanda juu wakiwacha pengo la pointi sita.
City ilitishia kusawazisha bao kwa kuvunja safu ya ulinzi ya Leicester huku mabeki wao wakionekana kutatizwa na washambuliaji wa Leicester.
Mahrez alifunga bao la pili huku Huth akifunga bao la tatu na kufanya mambo kuwa 3-0 kabla ya Sergio Aguero kuipatia City bao la kufutia machozi kunako dakika za mwisho.
Leicester ilikuwa imeishinda Tottenham iliopo katika nafasi ya tatu lakini ni ushindi huu dhidi ya Manchester City ambao umekuwa muhimu sana kwao.
Mbweha hao sasa wamechukua pointi 28,licha ya kupokonywa ushindi wa sita katika mechi zao saba.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.