ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 27, 2016

KILIPONUKA HII LEO:- BAADHI YA WABUNGE WAAMRIWA KUTOKA BUNGENI DODOMA.

**DRIVE MiX** 93.7 JEMBE FM KWA HEWA Yaliyojiri bungeni KIMENUKA ➖Askari imebidi waingie bungeni na baada ya mzozo wa mda mrefu wapinzani wote wakaamua kutoka nje . . ➖Baadhi ya Wabunge waliamriwa watolewe akiwemo Lissu . . ➖Wabunge wa Upinzani wakashkana mikono na kusema hawatoki
Mwenyekiti Chenge asema baada ya Dakika 10 wataendelea na kazi, hali itulie kwanza mjengoni.
KAULI YA SERIKALI KUHUSU TBC KUTANGAZA MOJA KWA MOJA MAJADILIANO YA VIKAO VYA BUNGE. Shirika la Utangazaji Tanzania TBC lilianza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania mwaka 2005. Kabla ya kuanza kurusha moja kwa moja TBC wakati huo Televisheni ya Taifa, ilikuwa inarekodi matukio yote ya Bunge na kurusha usiku katika vipindi maalum vilivyojulikana kama Bungeni Leo kwa maana ya yaliyojiri ndani ya ukumbi wa Bunge kwa siku husika. Baada ya kuanza kwa utaratibu wa kurusha matangazo moja kwa moja mwaka 2005 gharama za kufanya kazi hiyo zimekuwa zikipanda kwa kasi hadi kufikia Shilingi Bilioni 4.2 kwa mwaka (mikutano minne ya Bunge). Shirika limekuwa likigharimia kwa sehemu kubwa matangazo hayo kwa kutumia mapato yake yanayotokana na matangazo madogo ya biashara. Ifahamike kuwa Asilimia Sabini na Tano ni vipindi vingi vinavyolenga kutoa elimu kwa umma na asilimia ishirini na tano ni burudani. Kutokana na hali hii TBC imeona kuwa ni busara kubadilisha mfumo wa utangazaji wa shughuli za Bunge ili kukabiliana na kuzidi kupanda kwa gharama za uendeshaji. Hivyo basi TBC imeona ni busara kuanzia Mkutano huu wa Bunge iwe inarusha baadhi ya Matangazo ya Bunge moja kwa moja (Live) ikiwa ni njia ya kubana matumizi. Chini ya utaratibu huu TBC itahakikisha kuwa baadhi ya matukio ya Bunge yatarushwa moja kwa moja na mengine kurekodiwa na kuandaliwa kipindi maalumu kitakachoitwa LEO KATIKA BUNGE. Kipindi hicho kitakuwa na mambo yote muhimu yaliyojiri ndani ya Bunge kwa siku husika. Kipindi hicho kitakuwa kinarushwa kuanzia saa nne usiku hadi saa tano usiku. Kipindi hicho kimeanza tarehe 26 Januari, 2016 yaani jana na tayari baadhi ya wananchi wameonesha kuridhishwa na utaratibu huu wa kuwa na kipindi maalumu usiku kuhusiana shughuli za Bunge. Uamuzi huu utapunguza gharama za uendeshaji kwa shirika na pia kwa kupitia kipindi cha LEO KATIKA BUNGE Watanzania walio wengi watapata nafasi ya kufahamu yale yaliyojiri Bungeni kwani wakati Bunge linaendelea na mijadala yake Watanzania walio wengi huwa wanakuwa na kazi za kiofisi au zingine za ujenzi wa Taifa kwa mahali walipo.
CHENGE ASEMA "SAKATA LA ESCROW LIKIJA BUNGENI NITAKAA PEMBENI" **DRIVE MIX** 93.7 JEMBE “Katika Bunge lililopita, chama chako na wabunge walikuwajibisha kwa kashfa ya Escrow, je, siku ukiliongoza Bunge na hoja ikarudi ndani uko tayari kuisimamia,” Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe (Chadema) alimuuliza Chenge.
Akijibu swali hilo, Chenge alisema Bunge linaongozwa na Kanuni na itakapokuja mbele ya Bunge au kwenye Kamati, ikaonekana kuna maslahi ama inamhusu mbunge, ni busara kuzingatia kanuni nafasi hiyo ikaachwa mwingine aifanye shughuli za Bunge zisiwe na makandokando ya aina yoyote.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.