Baadhi ya Washiriki wa Mdahalao huo wakifuatilia mada iliyokuwa ikijadiliwa wakati wa mdahalo. |
Nchi mbalimbali duniani zimekuwa na sera mahususi kwa ajili ya
kukaribisha wawekezaji mbalimbali kuja kuwekeza kwenye nchi zao ili kuweza
kupata kipato kupitia kodi mbalimbali na faida nyingine kama ajira kwa wenyeji,
uboreshwaji wa miundo mbinu n.k. Moja ya nchi hizoni pamoja naTanzania.
Tanzania ilibadilisha sera zake za kiuchumi mwanzoni mwa miaka ya 1990, kwa kutoa fursa kwa sekta binafsi kuweza kumiliki uchumi. Sera hii ilivutia wawekezaji wengi toka nje na ndani kuwekeza katika sekta mbalimbali, moja ya maeneo ambayo wakezaji wamejikita ni sekta ya madini. Shinyanga ni moja kati ya mikoa yenye utajiri mkubwa wa madini nchini na hivyo kuvutia wawekezaji wakubwa katika sekta hiyo. Mfano mzuri ni kampuni ya Barrick inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani humo.

Mgodi huo unazungukwa na vijiji vitatu ambavyo ni Mwendakulima, Mwime
na Chapurwa. Lakini kutokana na hali
halisi kumekuwa na kelele nyingi za manung’uniko toka kwa jamii zinazoishi karibu
na maeneo hayo kuachwa bila maendeleo yoyote wakati wageni wanachukua madini
kwa kiwango ambacho hakijulikani.“Kitu kingine uwepo uwazi waweke uwazi katika
haya masuala ya madini mapato wamepata kiasi gani wawekezaji na serikali
yenyewe imepata kiasi gani, ikibidi hata kwa wale wananchi wanaozunguka mgodi huu
au migodi mingine ya Tanzania.
Waweze kuwa wanawabandikia kwamba mwezi huu mgodi umeingiza kipato hiki na serikali imepata hiki angalau kidogo inaweza kupunguza manung’uniko.
Kwa watanzania wengine ambao wanaishi sehemu ambapo hapana madini wapeleke hata kwenye magazeti matangazo ya mapato,” anafafanua mkazi wa Mwime.Haya yamejiri kwenye mda- halo uliondaliwa na waraghabishi wa Chukua Hatua toka kijiji cha Mwime. Ambapo wananchi walipata fursa yakuchangia mawazo kama madini ni laana ama neema.
Katika mdahalo huo ambao ulifanyika katika shule ya sekondari ya Mwendakulima washiriki toka kada mbalimbali za kijamii Kama wachungaji, mashekhe, wakulima, walimu, watendaji wa vijiji, wanafunzi na waandishi wa habari walipatafursa ya kuchangia mawazo yao kama madini ni laana ama neema.
Mwanafunzi wa kike toka katika shule ya sekondari ya Mwendakulima yeye aliona kwamba madini yanaweza yakawa ni janga la mazingira pale aliposema kwamba, “Suluhisho jingine angalau wangebadilisha mfumo wa uchimbaji, kwa sababu mfumo wanaotumia ule yaani kadri siku zinavyokuja kutakuwa na janga kubwa sana, angalia udongo uliofika pale huku chini kuna nini.” Ukiacha changamoto ya mazingira, suala jingine lililojitokeza ni athari zinazoletwa na kemikali mbalimbali ambapo mwalimu mraghabishi

Paul Chui wa shule ya msingi Mwime alisema, “Kwa kweli kutokana na sera ya elimu, bado tunafundisha elimu kwa
kuzingatia sera ya elimu. Hivyo kwa mimi kama mwalimu najitahidi sana
kuwaelekeza wanafunzi kuhusu suala zima la athari za kemikali kama vile
sunlight pamoja na mekyuri.” Wakati
washirki wengine waliojitokeza wao walielezea tatizo la kiungozi na mikataba
mibaya.
Katika kuelezea tatizo hilo walielezea usiri uliopo kwenye mikatabana hivyo kushauri wananchi kuhusisha siasa na mali zao kwa kuhakikisha kwamba wakati wa kupiga kura ni wakati sahihi wa kudhibiti maliasili za umma kwa kuchagua viongozi wanaofaa. Mapungufu katika sera pamoja na sheria za madini ni moja ya sababu zilizotajwa kufanya madini yaonekane laana kwa wananchi wanaozunguka migodi hiyo.

Katika maelezo yake kwa washiriki,
George Kingi ambaye ni mtendaji wa kijiji cha Mwime alisema, “Kuna mapungufu
kwenye sheria zetu hata ungemweka leo mwingine hata kila siku kama sheria hujaiboreshwa bado unarudi kulekule kwa hiyo
suala la sheria lifanyiwe marekebisho.
Kingine ni sera. Sera kama haisemi Mwime waachiwe asilimia fulani, hata ungemleta mwingine kesho na mwingine atakwamishwa na sera ambayo haisemi wanamwendakulima mbaki na nini.” Katika hili ushauri uliotolewa ni wa kukaa vikao wananchi wanatakiwa kutoogopa na wanapokaa kwenye vikao kweli wasema.

Kwa kuwa kama kuna watu wa kupiga
kelele kule juu sheria na sera zibadilishwe na zikabadilishwa basi kila kitu
kitakuwa sawa. Kama anavyomalizia George, “Ukishabadilisha sheria na sera hata maji
Mwime unayapata hata gari unaletewa si sera inasema uletewe gari kama sera
haisemiutaletewa gari?” Akitoa majumuisho ya mdahalo huo
uliondaliwa na waraghabishi walimu na wakulima Toka kijiji cha Mwime,
mwenyekiti Maimuna Said alisema “Madini
sio laana lakini viongozi wenyewe ni laana kwa sababu hawatendi haki ipasavyo
kulingana na katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania.
Hii ni neema toka kwa Mungu.” Suala jingine ambalo limejitokeza katika mdahalo huo ni wananchi kutokuwa na furaha jinsi ambavyo serikali haiwashirikishi katika kufanya maamuzi muhimu yanayohusu mustakabali wa maeneo yao. Hivyo ili madini yasiwe laana ni muhimu sana kwa serikali kuwashirikisha wananch toka hatua za mwanzo.

Lakini pia suala zima la kutoa elimu ya uraia kwa wananchi. “Kuna haja kubwa ya kutolewa elimu hususani
elimu ya uraia. Watu kwanza watambue haki zao, mtu akishatambua haki zake kuna
kuwa na uwezekano wa yeye kuzidai, lakini kama watu bado hawatapata elimu hiyo
ni kwamba watu watakuwa wananung’unika tu pembeni. Lakni hajui aanzie wapi na
hajui aishie wapi,” anafafanua Maalim Daudi Athman Imamu wa Masjid Noor
Nyandekwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.