WASHINDI 16 wapatikana katika droo ya Airtel Mkwanjika Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imechezesha droo ya kwanza ya promosheni ya Airtel Mkwanjika na kuwapata washindi 16 wa siku nne za mwanzo Promosheni ya Airtel Mkwanjika imezinduliwa na Airtel wiki iliyopita ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja wake katika msimu huu wa siku kuu za mwisho wa mwaka na X-mass ambapo jumla ya shilingi milioni 300 zimetengwa na kampuni hiyo kushindaniwa na wateja wake kama zawadi.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa droo hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Airtel Mkwanjika leo tumewanyakuwa washindi 16 wa siku nne za mwanzo ambapo kila siku ni washindi wanne na kila mmoja ataweza kujizolea hadi shilingi milioni moja katika boksi letu la Airtel Mkwanjika .
Mmbando aliwataja walioibuka washindi wa kuingia katika boksi la Airtel Mkwanjika kuwa Mama Masisimba , Abdallah S Rashid, Amani Maruma, Msafiri Saidi Ruwia , Hassani Hamis Suleyman na Aida Asabwile Mwafi wakazi wa mkoa wa Dar, es salaam. Carston Magoah na Godfrey Frank Kamota wakazi wa Morogoro, Hassan Ngakoma mkazi wa Manyara , Safari Aidaru mkazi wa Mbulu, Lupembe Massanja kutoka Rufiji , Rachel Obedi Muhumu mkazi wa Moshi na Rodrique kimei mkazi wa Msumbiji.
Washindi hawa watapigiwa simu na kupatiwa maelekezo zaidi jinsi ya kupata na kupoke zawadi zao. Nae Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga alisema “Promosheni yetu imeanza kufanikiwa kwa kuwa tayari tumewapata wateja wetu 16 na tumeshaandaa jumla ya milioni 16 ilikila mmoja akishajizolea pesa kwenye sanduku la pesa papo hapo tutampatia pesa yake aliyokusanya kupitia Airtel Money ili akasherehekee sikukuu kwa furaha zaidi”
Promosheni ya “Airtel MKWANJIKA” itawawezesha wateja wote wanaojinga na kifurushi chochote cha yatosha au kuongeza muda wa maongezi wa kiwango chochote kwenye simu zao kuingia moja kwa moja kwenye droo ya siku na kupata nafasi ya kujishindia pesa taslimu
Hakuna gharama ya ziada wala malipo yeyote unaongeza salio kwa kutumia vocha, huduma ya Airtel money au kununua vifurushi vya yatosha na kujishindia pesa kila siku” alisisitiza Muga.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.