Mshindi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Msimu wa nne Bi. Caroline Chelele aliyekaa kwenye Pawatila akifurahia zawadi zake, Muda mfupi baada ya kukabidhiwa.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombelo Bw. Yahya Naiya (wa pili kushoto) aliye muwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo akikata utepe kuashiria tukio la kumkabidhi zawadi rasmi mama shujaa wa chakula msimu wa nne 2015 Bi. Caroline Chelele, wa kwanza kushoto ni Mercy Minja Kaimu mkurugenzi wa wa mji wa Ifakara, wa tatu kutoka kulia ni Mama Shujaa wa Chakula Bi. Caroline Chelele na Mbunge wa Jimbo la Kilombelo Mh. Peter Lijuakali
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombelo Bw. Yahya Naiya (wa pili kushoto) aliye muwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo akimpongeza Mama shujaa wa chakula 2015 baada ya kukabidhiwa zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tsh Milioni Ishirini(20,000,000)
Vifaa vya kilimo ambavyo alikabidhiwa mama Shujaa wa Chakula Msimu wa nne 2015, ikiwa ni Pawatila na Mashine ya kumwagilia na Shamba lenye Hekta 7 ambalo halipo pichani.
Mshindi wa Shindano la Mama shujaa wa chakula linalo endeshwa na Oxfam kupitia Programu yake ya Grow Bi Caroline Chelele akitoa neno la Shukurani baada ya kukabidhiwa zawadi.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombelo Bw. Yahya Naiya (wa pili kushoto) aliye muwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo, akitoa neno la shukurani kwa Shirika la Oxfam kwa jinsi wanavyo wajali na kuwawezesha wakulima wadogo wadogo.
Mbunge wa Kilombelo Mh. Peter Lijuakali akimpa pongezi mama shujaa wa Chakula 2015 kwa kuleta ushindi mkubwa wilayani hapo na kuwasihi akinamama wengine wajitokeze kushiriki kipindi ambacho nafasi inatokea tena na kurudisha ushindi huko.
Meneja wa Ushawishi na utetezi kutoka Oxfam Eluka Kibona akielezea kwa undani kuhusiana na shindano la Mama shujaa wa Chakula.
Mtaalam wa Kilimo hai kutoka SOAM wa tatu kutoka kushoto akitoa maelezo ya namna ya kutengeneza mbolea asiyo na kemikali yoyote kwa kutumia Majani,Magugu, Majivu,Maji na Udongo
Baadhi ya wanakijiji wakifanya kazi kwa vitendo kwa kusombelea nyasi kavu pamoja na magugu kwa ajili ya kutengeneza Biwi
Shamba darasa la utayarishaji wa Biwi likiwa linaendelea
Baadhi ya wanakijiji ambapo mama Shujaa wa Chakula alipokabidhiwa zawadi zake, wakifuatilia kwa makini shamba Darasa
Mshindi wa shindano la Mama Shujaa wa chakula 2015 msimu wa nne Bi. Caroline chelele (Kulia) akimkabidhi zawadi Kaimu Mkurugenzi wa Mji wa Ifakara Bi. Mercy Minja kwa niaba ya Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombelo
Bi.Caroline chelele akikabidhi zawadi yake ya Kigoda kwa Shirika la Oxfam, kutoka kushoto ni Narsis Silvesti, Eluka Kibona na wa kwanza kulia ni Suhaila Thawer wote kutoka Oxfam Tanzania
Mama Shujaa wa chakula akikabidhi zawadi ya Picha kwa Shirika la Oxfam
Watalam wa Kilimo hai kutoka SOAM wakimkabidhi vipeperushi vinavyozungumzia kilimo hai Mama Shujaa wa Chakula 2015 Bi. Caroline Chelele
Baadhi ya wananchi waliokuwa katika sherehe hizo za kukabidhiwa zawadi mama shujaa wa Chakula.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Wilaya ya Kilombelo, Shirika la Oxfam na Mshindi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Msimu wa nne 2015 Bi.Caroline Chelele
Mshindi wa
shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015, Linaloendeshwa na Shirika la Oxfam
kupitia program yake ya Grow msimu wa nne Caroline Chelele amekabidhiwa zawadi
ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya kiasi cha shilingi Millioni 20, nyumbani
kwake kata ya Ifakara mkoani Morogoro.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo ya
zawadi Mkoani Morogoro wilayani
Kilombero kata ya Ifakara,Meneja Ushawishi na Utetezi kutoka Shirika la
Oxfam,Eluka Kibona alisema zawadi hiyo ni moja ya utekelezaji wa shindano hilo
kwa mshindi aliyeshinda shindano hilo la Mama shujaa wa Chakula 2015.
Alisema shirika lao linatoa takribani Milioni 20
kwa mshindi ambapo mshindi anatakiwa
kuchagua zawadi ya vifaa vya kilimo ili kuweza kumuwezesha zaidi. Kibona
alisema Mshindi huyo alikabidhiwa Pawatila kwa ajili ya kubebea Mazao,vifaa vya
umuagiliaji pamoja na Shamba lenye Ekali 7. "Huu ni muendelezo wa shindano
la mama shujaa wa Chakula kukabidhi zawadi kwa ajili ya kuwainua wakulima
wadogo wadogo kuonekana na Serikali kama wao wanamchango mkubwa kwa jamii
kutokana na Chakula wanacholima ndicho kinacholisha taifa,"alisema Kibona
. Aliongeza shindano hilo lipo chini ya Kampeni ya GROW yenye lengo la kuwainua
wakulima wadogo wanaokumbana na changamoto mbalimbali katika kilimo.
Kwa Upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya
Kilombero , Yahya Naniya aliishukuru shirika hilo kwa hatua ya kuwathamini na
kuwapigania wakulima wadogo ambao asilimia kubwa kati yao ni wanawake.Alisema
kupitia shindano hilo linaweza kuongeza Chachu kwa wakulima kufanya
shughuli za kilimo kwa kasi na kuongeza wigo mpana wa kupata mazao mengi
kutokana na Mashirika mbalimbali kuwawezesha.
Naye Mshindi wa Shindano hilo 2015,Caroline
Chelele alisema atahakikisha zawadi hizo anazifanyia kazi ipasavyo
itakayomuwezesha kumuongezea mazao mengi zaidi. Aliomba Serikali pamoja na
mashirika mbalimbali kuendelea kuasidia wakulima wadogo na kuhakikisha nao
wanathaminiwa kama wakulima wakubwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.